|
Mapema Leo-Wa tatu kutoka kulia ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akiwasili katika kijiji cha Negezi kata ya Mwawaza katika manispaa ya Shinyanga kuangalia nama ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga ikiwa ni katika kukagua utekelezaji wa ilani ya ccm ya mwaka 2010.Mgeja alikuwa amembatana na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Shinyanga,watendaji wakuu wa serikali ya
mkoa,mkuu wa mkoa,wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri(wengi hawapo pichani)
|
|
Msafara baada ya kuwasili katika eneo la mradi wa ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga ulioanza mwezi Machi mwaka huu,ambapo sasa zoezi la kuchimba misingi kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala ukiwa unaendelea ,na hadi kukamilika kwa mradi huo karibia bilioni mia moja zinahitajika |
|
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akizungumza leo katika eneo kunakojengwa hospitali ya rufaa ya mkoa ambapo alisema
hospitali hiyo ya rufaa ambayo imeanza kujengwa mwezi Machi mwaka huu na sasa uchimbaji
wa misingi kwa ajili ya jengo la utawala unaendelea na hadi kukamilika kwa ujenzi wa hospitali hiyo takribani shilingi bilioni mia moja zinahitajika huku akiwataka wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo wananchi kushiriki kufanikisha ujenzi huo.
|
|
Katikati ni mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akizungumza katika eneo la mradi ambapo alisema kutokana
na mradi huo mkubwa na wa kihistoria katika mkoa wa Shinyanga ni vyema serikali
inayoongozwa na rais Jakaya Kikwete ikaliona suala la ujenzi huo kama la
dharura kwa kuweka fungu kubwa la fedha badala ya shilingi bilioni moja kama
ilivyofanya awamu hii. Mgeja alisema kukamilika kwa ujenzi huo kutasaidia kwa kiasi kikubwa hivi sasa wananchi wanapata adha kubwa
katika kupata huduma za matibabu ambapo hospitali ya mkoa wa
Shinyanga imeelemewa ambapo kitanda kimoja kinatumiwa na wagonjwa zaidi ya mmoja. |
|
Wa pili kutoka kulia ni mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akizungumza katika eneo la mradi wa ujenzi wa hospitali ya mkoa ambapo alisema jumla ya hekari 135 zimetengwa kwa ajili ya hospitali
hiyo ambao unatarajia kukamilika ndani ya miaka 5 hadi 6 kama pesa nyingi
zitatengwa kwa ajili ya mradi huo ambapo sasa mkoa umetengewa shilingi bilioni
1 na tayari wameshapokea milioni 500 kwa ajili ya ujenzi huo.
|
Zoezi la kuchimba misingi likiwa linaendelea ambapo imeelezwa kuwa ujenzi wa hospitali rufaa ya mkoa wa Shinyanga utakamilika ndani ya miaka 5 hadi 6 kutokana na changamoto ya pesa iliyopo kufanikisha ujenzi huo.
Picha zote na kadama malunde wa malunde1 blog
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com