|
Makamu mkuu wa chuo kikuu cha mtakatifu Agustino(SAUT) taaluma Padri Dkt.Thadeus Mkamwa ,akizungumza kwenye tafrija fupi ya kuwaaga wahitimu wa kozi ya habari za uchunguzi za biashara,kilimo na uchumi(Investigative business Journalism) katika ukumbi wa chuo hicho jana. Aliwataka wahitimu kuhakikisha wanaleta mabadiliko katika sekta hiyo kwa kuandika habari ambazo zitakuwa zimefanyiwa utafiti na uchunguzi wa kina kupitia mafunzo waliyoyapata ili kuleta mabadiliko katika jamii. |
|
|
| |
Mkurugenzi wa utafiti kutoka shirikisho la viwanda Tanzania (CTI) Hussein Kamote ,aliwataka waandishi wa habari waliohitimu kozi hiyo,kufanya kazi kwa kushirikiana na wajasiliamali na CTI kwa kuwa wao wanatakwimu nyingi ambazo zinaweza kusaidia kufanikisha kazi zao vizuri,kwani waandishi wanafanya kazi kubwa ya kushawishi ili kuboresha mazingira ya biashara.
Project manager kutoka Best AC Ali Mjella, akiwaasa wahitimu kuutumia ujuzi walioupata kutoa msukumo zaidi katika kuangalia changamoto zilizopo, kwenye biashara na mazingira yake kwa ujumla likiwemo suala la miundombinu ya barabara,masoko na vikwazo vingine vinavyochangia kuchelewesha maendeleo.
|
Mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya kozi ya Investigative Business Journalism (IBEJ) Stella Ibengwe akisoma risala ya wahitimu kwa mgeni rasmi ambaye ni makamu mkuu wa chuo cha SAUT taaluma Padri Thadeus Mkamwa.
|
|
Mhadhiri kutoka chuo cha SAUT Anne Gongwe ,akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake kutokana na waandaji wa kozi hiyo Best AC,ANISAF na SAUT, kuwaamini na kuwateuwa kufundisha kwa kuwa waliona wanafaa na uwezo wa kutosha. |
|
Mkurugenzi wa ANISAF Audax Rukonge anawataka wahitimu kuifanyia kazi elimu waliyoipata, ili kuleta mabadiliko ya kisera na sheria zitakazo saidia kuboresha mazingira ya kilimo na biashara Tanzania. |
|
Hongera kijana Felix Razaro kwa kuhitimu kozi ya (IBEJ). |
|
Makamu mkuu wa chuo cha SAUT Padri Dkt.Thadeus Mkamwa akimkabidhi cheti mhitimu Stella Ibengwe. |
|
Kutoka kulia ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es salaam Dkt Goodluck Urassa,anayefuata ni makamu mkuu wa chuo cha SAUT taaluma, Padri Thadeus Mkamwa,project meneja wa Best AC Ali Mjella na wa kwanza kushoto ni kutoka shirikisho la viwanda Tanzania (CTI) Hussein Kamote wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa tafrija fupi ya kuwapongeza wahitimu wa kozi ya (IBEJ). |
|
Moses mathew akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi kwa niaba ya wahitimu wote,mara baada ya kukabidhiwa vyeti. |
|
Hongera Nancy Ijumba kwa kuhitimu masomo yako,tunakutakia mafanikio mema. |
|
Anna Luhasha akikabidhiwa cheti chake na makamu mkuu wa chuo SAUT taaluma Dkt. Mkamwa mara baada ya kuhitimu kozi ya Investigative business Journalism. |
|
Ni furaha na kicheko baada ya kuhitimu |
|
Baadhi ya wahitimu wa kozi ya IBEJ wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi kutoka chuo cha SAUT,Best AC,ANSAF, ambao ndiyo waandaaji wa kozi hiyo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika kuhakikisha wanaripoti kwa kina habari za kilimo na biashara. |
PICHA ZOTE KWA HISANI YA STELLA BLOG
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com