Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Ukatili!! BABA AUA MTOTO WAKE WA MIAKA MITATU KWA KIPIGO,KISA NI MKOROFI HAMSIKILIZI BABA YAKE

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita-Joseph Konyo
Ukatili dhidi ya watoto umeendelea kutokea katika jamii ambapo mtoto James Wilson(3)mkazi wa kijiji cha Misri kata ya Bugalama wilayani Geita mkoabi Geita ameuawa kwa kupigwa baba yake mzazi kwa madai kuwa mtoto huyo amekuwa hamsikilizi baba yake kwa sababu ya ukorofi.

Akizungumzia tukio hilo diwani wa kata ya
Bugalama Samweli william amesema baba mzazi wa mtoto huyo Wilson Chimba(46) alimtuma mtoto kununua mafuta alipokataa akaanza kumpiga.

Kufuatia kipigo hicho mtoto huyo alikwenda kujificha kwa jirani yake na siku iliyofuata baba mzazi alipomfuata mtoto huyo kisha kumpiga hadi kumuua.

 Jeshi la polisi mkoani Geita limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba tayari limemkamata mtuhumiwa huyo kwa kitendo hicho cha kinyama.

Na Valence Robert wa Malunde1 Blog-Geita


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com