Kamanda wa polisi mkoa wa Geita-Joseph Konyo |
Ukatili dhidi ya watoto umeendelea kutokea
katika jamii ambapo mtoto
James Wilson(3)mkazi wa kijiji cha Misri kata ya Bugalama wilayani Geita mkoabi Geita ameuawa kwa kupigwa baba yake mzazi kwa madai kuwa mtoto huyo amekuwa hamsikilizi baba yake kwa sababu ya ukorofi.
Akizungumzia
tukio hilo diwani wa kata ya
Bugalama Samweli william amesema baba mzazi wa mtoto huyo Wilson Chimba(46) alimtuma mtoto kununua mafuta alipokataa akaanza kumpiga.
Bugalama Samweli william amesema baba mzazi wa mtoto huyo Wilson Chimba(46) alimtuma mtoto kununua mafuta alipokataa akaanza kumpiga.
Kufuatia
kipigo hicho mtoto huyo alikwenda kujificha kwa jirani yake na siku iliyofuata
baba mzazi alipomfuata mtoto huyo kisha kumpiga hadi kumuua.
Jeshi la polisi mkoani Geita limethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kwamba tayari limemkamata mtuhumiwa huyo kwa kitendo
hicho cha kinyama.
Na
Valence Robert wa Malunde1 Blog-Geita
Social Plugin