Ukatili Uliopitiliza Geita!! MTOTO WA MIAKA 8,ABAKWA,AZIBWA MDOMO NA SEHEMU ZA SIRI KWA NGUO,KISHA KUNYONGWA

Katika hali ya kusikitisha na kutia simanzi, mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Kalangalala mjini Geita aitwaye Magreth Kervini(8)  amebakwa na kufungwa nguo mdomoni na sehemu za siri kisha kunyongwa shingo  hadi kufa na kutupiwa uvunguni mwa kitanda usiku wa kuamkia leo katika mtaa wa Nyerere mjini Geita.

Tukio hilo lililoshangaza watu wengi mjini Geita
limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa 8 usiku  ambapo mmoja kati ya walioshuhudia tukio hilo amesema usiku huo kulikuwa na ugomvi kati ya mpangaji mwenzake aitwaye Shida ambaye alikuwa analazimishwa kufanya mapenzi kwa lazima na shemeji zake  wawili ambao ni Kurwa  Juma na Dotto Juma(30-35) ambaye ni mke wa mdogo wao Shija Juma.

Shuhuda huyo aliendelea kusimulia  kuwa mpangaji huyo (mme wa Shida) Shija siku hiyo alikuwa ameenda kulala kwa mke mwingine katika maeneo ya Bomani lakini kufuatia ugomvi uliokuwa ukiendelea nyumbani kwake, alipigiwa simu na mdogo wa mke wake anayekaa naye huko mtaa wa Nyerere na kuambiwa kuwa wadogo zake wamekuja nyumbani na wamo ndani wanafanya fujo wanataka kumbaka yake dada yake(Shida).

Mara baada ya kupata taarifa hizo Shija aliondoka alikokuwa amelala akapanda pikipiki hadi kwa mke wake Shida na alipofika aliwakuta ndugu zake (Kurwa na na Dotto) wamo ndani wakigombana na shemeji yao.

Kufuatia kitendo hicho Shija alianza kuwapiga Kurwa na Dotto hali iliyomfanya Dotto kutoka nje na kujificha  nje ya geti wakati huo huo ndani Kurwa na Shija wakiendelea kugombana.....

Kufuatia kipigo alichokipata,Kurwa naye alitoka nje na Shija baada ya kuona ndugu zake wametoka,mke wa Shija(Shida) alifunga mlango na akalala huku Shija akirudi kulala Bomani alikokuwa amelala awali.

Shuhuda huyo anasimulia kuwa....

“Baada ya muda mfupi Dotto alirudi baada ya kuona Kurwa na Shija wameondoka,
na ndipo akaenda kwenye mlango wa shemeji yake akakuta umefungwa na kuamua kuhamia kwenye mlango mwingine na ndipo alipogonga mlango huo akatoka mtoto Magreth Kervini (8)  kumfungulia kwani alijua kuwa atakuwa mama yake aliyekuwa ameenda kazini huenda amerudi kwani mama yake na mtoto Magreth anafanya kazi Makongoro bar.

Inadaiwa kuwa Dotto baada ya kufunguliwa mlango na Magreth Kervini,aliingia na kuanza kumbaka mtoto huyo na baada ya kutekeleza adhima yake alimnyonga  hadi kufa na akamfunga nguo mdomoni na sehemu za siri akatoka nje na alipotoka nje alienda tena kwenye mlango wa nyumba nyingine ya mama Mulugu Nyamuhanga ili akafanye unyama mwingine.


Baada ya muda mfupi  mama huyo Mulugu Nyamuhanga alisikika akipiga kelele za kuomba msaada kwamba amevamiwa na majambazi majirani walitoka nje wakakuta mlango wa binti huyo ukiwa umefunguliwa na walipoangalia walikuta binti huyo akiwa amefungwa kanga na damu zikitoka sehemu za siri akiwa amekufa.

Hata hivyo kuna na tetesi kuwa mama mzazi wa mtoto aliyeuawa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Dotto.

Kwa upande wa mama yake mzazi  Peki Makoye (29) hakuwepo nyumbani na hakuwa na mawasiliano ya simu, alikuwa kazini.

 Alisema hana uhusiano wowote wa kimapenzi na Dotto bali ana uhusiano na Kurwa na kuongeza kuwa huenda Dotto ndiye amefanya unyama huo kwani alishawahi kumtaka kimapenzi na akakataa.

Mpasa sasa hivi Shija,Kurwa na Shida wanashikiliwa na jeshi la polisi.

Kamanda wa polisi mkoani Geita kamishina msaidizi Joseph konyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na uchunguzi bado unaendelea ili hatua zaidi zichukuliwe



Na Valence Robert-wa Malunde1 blog Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post