Updates!! WALIOBUGIA POMBE HARAMU HUKO KENYA WAENDELEA KUPOTEZA MAISHA SASA ZAIDI YA 70,WENGINE WALIPOTIWA KUPOTEZA UWEZO WA KUONA

Watu wawili wamekamatwa nchini Kenya kuhusiana na mkasa wa watu zaidi ya 70 kufariki kutokana na kunywa pombe iliyokuwa imetiwa sumu.

Vifo hivyo vimetokea katika muda wa saa 48 baada ya walevi kuanza kulewa siku ya Jumapili na Jumatatu asubuhi.

Madaktari wanafanya kila wawezalo kujaribu kuokoa baadhi ya waathiriwa ambao wamelazwa hospitalini.

Pombe hiyo iliyopewa jina la 'Countryman', inasemekana iliwekwa sumu aina ya Methanol na kusababisha baadhi ya waliokuwa wamekwenda kuibugia kufariki huku wengine wakisalia hali mahututi na wengine kupoteza uwezo wao wa kuona.

Vifo hivyo vilianza kutokea mapema wiki hii katika mkoa wa kati na katika eneo la Mashariki mwa Kenya.

Inaarifiwa wengine wengi wamelazwa hospitalini baada ya kubugia pombe hiyo.

Idadi ya vifo ilianza kuongezeka huku watu wengine 14 wakifariki katika jimbo la Embu Mashariki mwa nchi , wengine wanne wakifariki katika jimbo la Makueni. Watu 75 wamelazwa hospitalini katika jimbo hilo wengine watatu wakiripotiwa kupoteza uwezo wao wa kuona.

Kwa sasa wataalamu wanafanyia utafiti kinywaji hicho pamoja na mkojo kutoka kwa wagonjwa kubaini kilichowekwa ndani ya pombe hiyo.

Matokeo yanatarajiwa katika siku mbili zijazo.


Hadi sasa watu 76 wanasemekana kufariki kutokana na pombe hiyo katika maneo mbali mbali ya nchi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post