Usitake Kusimuliwa!!! FUATILIA HAPA TUKIO ZIMA LA MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI MKOANI SHINYANGA


Ni katika ukumbi wa Diamond Fields Hotel mjini Shinyanga ambako kumefanyika sherehe ya uhuru wa vyombo vya habari katika mkoa wa Shinyanga ambako waandishi wa habari zaidi ya 30 kutoka mkoani Shinyanga pamoja na wadau wa habari mkoani humo wamejumuika pamoja katika siku hii muhimu ambayo hufanyika Tarehe 3 mwezi Mei kila mwaka kote duniani,lengo likiwa kuhamasisha utendaji kazi kwa vyombo vya habari pamoja na kuhamsisha na kuimbusha serikali na jamii kwa ujumla kuhusu umuhimu wa vyombo vya habari.

 Waandishi wa habari wakiwa katika ukumbi wa Diamond Fields Hotel wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani ambapo kauli mbiu mwaka huu inasema “Uhuru wa habari kwa maendeleo na utawala bora”.

Waandishi wa habari pamoja na wadau wa habari mkoa wa Shinyanga wakiwa wameinamisha vichwa chini na kukaa kimya kwa muda wa dakika moja kuwakumbuka waandishi wa habari waliotangulia mbele za haki

Katibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Kareny Masasy akizungumza katika sherehe hizo ambapo alisema klabu hiyo ilianzishwa mwaka 2003 na ina jumla ya waandishiwa habari 31,huku akiitaka jamii kuendelea kushirikiana na waandishi wa habari mkoani humo katika kufanikisha maendeleo na utawala bora.
Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (SPC) Shija Felician akifungua sherehe za maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo ambapo waandishi wa habari pamoja na wadau wa habari  wamehudhuriakatika maadhimisho hayo.

Mshereheshaji katika sherehe za maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari mkoa wa Shinyanga Bi Veronica Natalis ambaye ni mwandishiwa habari na mtangazi kutoka Radio Faraja akifanya yake katika ukumbi wa Diamond Fields Hotel mjini Shinyanga

Sherehe zinaendelea ambapo waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga walimpongeza mkuu wa upelelezi mkoa wa Shinyanga Hussein Kashindye kwa ushirikiano wake na vyombo vya habari

 Waandishi wa habari wakifuatilia kilichokuwa kinajiri-Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari katika mkoa wa Shinyanga alikuwa meneja wa benki ya CRDB mkoa wa Shinyanga Said Pamui.
Mgeni rasmi katika sherehe hizo meneja wa benki ya CRDB mkoa wa Shinyanga Said Pamui akizungumza katika sherehe za leo ambapo aliwaasa waandishi wa habari kujituma katika kutafuta habari pamoja na kwamba kuna baadhi ya wadau hawatoi ushirikiano kwao kwa kuficha habari huku akiwataka kuendelea kuwa na mahusiano mazuri na jamii

Mkuu wa upelelezi mkoa wa Shinyanga Hussein Kashindye akizungumza wakati katika sherehe hizo ambapoa pamoja na mambo mengine aliwataka waandishi wa habari kuandika habari zinazogusa jamii nzima badala ya kuandika habari zinazohusu mtu mmoja na kuwataka waandishi wa habari kuunga mkono kampeni aliyoianzisha ya “Vikongwe na makazi salama”.

Kaimu afisa uhusiano mamlaka ya maji safi na mazingira katika manispaa ya Shinyanga(SHUWASA)bi Amina Mabula akichangia mawili matatu katika sherehe hizo ambapo aliwapongeza waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga kuwa mstari wa mbele kushirikiana na mamlaka hiyo

Aliyesimama ni meneja wa Radio Kahama,Marko Mipawa akizungumza katika sherehe hizo ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuna baadhi ya sheria zinabana uhuru wa vyombo vya habari hivyo kukwamisha shughuli za waandishi wa habari hasa pale wanapohitaji kutoa taarifa flani lakini sheria inazuia mfano taarifa kutoka jeshi la polisi ambazo msemaji pekee ni kamanda wa polisi wa mkoa husika.

Aliyesimama na mwandishi wa habari wa ITV na radio one bwana Stephen Wang'anyi akizungumza katika sherehe hizo,ambapo alisema moja ya changamoto wanazokabiliana nazo waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ni kukosa ushirikiano wa karibu na jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ambapo kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga amekuwa mgumu wa kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari

Aliyesimama ni meneja wa Radio Faraja bi Moshi Abdallah Ndugulile akizungumza katika sherehe hizo ambapo aliiomba jamii kushirikiana na waandishi wa habari 

Aliyesimama ni bwana Chibura Makorongo akichangia mawili matatu kuhusu wadau wasioonesha ushirikiano kwa waandishi wa habari kama ilivyo hivi sasa kwa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ambaye amekuwa mgumu kutoa habari kwa waandishi wa habari  na wakati mwingine kusema hajui kuhusu matukio yanayoendelea katika mkoa hata kama askari polisi wake wapo katika eneo la tukio.

Mwenyekiti wa kamati ya maadili katika klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga James Thomas Makwinya ambaye ni wakili na mwanasheria wa manispaa ya Shinyanga,akitoa shukrani wakati wa kufunga sherehe hizo ambapo pamoja na kuwapongeza kwa kufanya kazi vizuri pia aliwataka wazingatie maadili ya kazi yao.


Picha ya pamoja waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali wa habari

Ilikuwa ni furaha mwanzo mwisho-Kila mtu alikuwa na furaha yake baada ya sherehe hizo kumalizika wengine wakadiriki kupiga picha ya pamoja kama unavyoona pichani,wa kwanza kushoto ni bwana Stephen Wang'anyi wa Itv na Radio One ,akifuatiwa na bi Kareny Masasy katibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,wa kwanza kushoto ni  Bi Stella Ibengwe mweka hazina wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم