Kutokana na tukio lililotokea jana (Aprili 30 mwaka huu) kwenye kambi ya timu ya Taifa (Taifa Stars) iliyopo Tukuyu mkoani Mbeya likihusisha usajili wa baadhi ya timu, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemteua Wakili Wilson Ogunde kuchunguza mlolongo mzima wa tukio hilo.
Baada ya kukamilisha uchunguzi wake, Wakili Ogunde ataishauri TFF kuhusu hatua za kisheria na kikanuni za kuchukua.
TFF inatoa wito kwa wachezaji, klabu na wadau wa mpira wa miguu kufuata kanuni na taratibu katika utendaji wao.
Domayo amesajiliwa na Azam FC akiwa kambini Taifa Stars mjini Tukuyu wakati timu hiyo inajiandaa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Malawi.
Usajili wake umezua gumzo huku TFF ikiendelea kusisitiza kwenye kambi za timu ya taifa si sehemu sahihi ya kufanya masuala ya usajili.
Social Plugin