WAFANYA USAFI WA MAZINGIRA KAHAMA WAFANYISHWA KAZI BILA MKATABA,WAACHISHWA KAZI BILA UTARATIBU


UMOJA wa wafanya usafi wa mazingira  katika halmashuri ya mji wa kahama mkoani shinyanga wameulalamikia uongozi wa Afya katika Halmashauri hiyo kwa kuwafanyisha kazi bila Mkataba wowote kinyume na Sheria ya Utumishi wa Umma.

Kauli hiyo  imetolewa juzi na Baadhi ya wafanya usafi wa Mazingira katika Halmashauri ya mji huo   juu ya utaratibu wa kufanya kazi kama  waajiriwa au wanafanya kazi  kwa mkataba.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanya usafi barabarani,maziku John alisema kuwa wanafanya kazi bila ya Mkataba wowote hali ambayo inapelekea kwa Baadhi ya Wafanyakazi kuachishwa kazi bila utaratibu wowote kitu ambacho ni tofauti na sheria ya Utumishi.

John aliendelea kusema kuwa halmashauri ya Mji inawalipa mshahara wa Shilingi laki moja kama Vibarua kwa kila mwezi kwa kuwapa mkononi ambapo alidai kuwa fedha hiyo haikidhi hata mahitaji yao ya kila siku.

Hata hivyo Wafanya usafi hao wakiongea kwa  nyakati tofauti walieleza kuwa pamoja na Halmashauri hiyo kuwalipa mshahara yao walisema endapo mfanyakazi ameugua anajigharamikia mwenyewe na kipindi wanapoenda Hospitalini kwa matibabu hawatambuliki kama wafanyakazi na kuelezwa kuwa si waajiriwa.

Kutokana na kufanya kazi pasipo na mkataba wowote imepelekea kwa baadhi ya wafanyakazi kufukuzwa holela na Afisa huyo wa Afya Masele katika sehemu yao ya kazi bila utaratibu wowote na kuweka wengine hali waliyodai kuwa huenda Rushwa imetendeka.

John aliwataja baadhi ya  wafagiaji wa Barabara za Mji huo kuwa  ni pamoja na Tatu Khamisi, Obed Samsoni,Eliyanzima Sehemu na Lucia Mabala  ambapo alisema kuwa ni wazoefu wa kazi hizo kwa miaka mingi tangu enzi za Halmashauri ya Wilaya.

Kwa upande wake Afisa Afya wa Mji ,Martini Masele,Mtanzania ilipomtafuta kwa njia ya simu yake ya kiganjani baada ya kumkosa Ofisini kwake alipokea simu alipohojiwa kuhusiana na malalamiko hayo alikata simu na kuifunga.

Via>>mohabmatukio blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post