UMOJA wa wafanya usafi wa mazingira katika halmashuri ya mji wa kahama mkoani shinyanga wameulalamikia uongozi wa Afya katika Halmashauri hiyo kwa kuwafanyisha kazi bila Mkataba wowote kinyume na Sheria ya Utumishi wa Umma.
Kauli hiyo imetolewa juzi na Baadhi ya wafanya usafi wa Mazingira katika Halmashauri ya mji huo juu ya utaratibu wa kufanya kazi kama waajiriwa au wanafanya kazi kwa mkataba.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanya usafi barabarani,maziku John alisema kuwa wanafanya kazi bila ya Mkataba wowote hali ambayo inapelekea kwa Baadhi ya Wafanyakazi kuachishwa kazi bila utaratibu wowote kitu ambacho ni tofauti na sheria ya Utumishi.
John aliendelea kusema kuwa halmashauri ya Mji inawalipa mshahara wa Shilingi laki moja kama Vibarua kwa kila mwezi kwa kuwapa mkononi ambapo alidai kuwa fedha hiyo haikidhi hata mahitaji yao ya kila siku.
Hata hivyo Wafanya usafi hao wakiongea kwa nyakati tofauti walieleza kuwa pamoja na Halmashauri hiyo kuwalipa mshahara yao walisema endapo mfanyakazi ameugua anajigharamikia mwenyewe na kipindi wanapoenda Hospitalini kwa matibabu hawatambuliki kama wafanyakazi na kuelezwa kuwa si waajiriwa.
Kutokana na kufanya kazi pasipo na mkataba wowote imepelekea kwa baadhi ya wafanyakazi kufukuzwa holela na Afisa huyo wa Afya Masele katika sehemu yao ya kazi bila utaratibu wowote na kuweka wengine hali waliyodai kuwa huenda Rushwa imetendeka.
John aliwataja baadhi ya wafagiaji wa Barabara za Mji huo kuwa ni pamoja na Tatu Khamisi, Obed Samsoni,Eliyanzima Sehemu na Lucia Mabala ambapo alisema kuwa ni wazoefu wa kazi hizo kwa miaka mingi tangu enzi za Halmashauri ya Wilaya.
Kwa upande wake Afisa Afya wa Mji ,Martini Masele,Mtanzania ilipomtafuta kwa njia ya simu yake ya kiganjani baada ya kumkosa Ofisini kwake alipokea simu alipohojiwa kuhusiana na malalamiko hayo alikata simu na kuifunga.
Via>>mohabmatukio blog