Kundi la wanaume watano akiwemo afisa mmoja wa polisi limedaiwa kuwabaka na kuwauwa wasichana wawili wadogo ambao ni ndugu katika mji mmoja nchini India na kisha kuining’iniza miili yao juu ya mti kwa mujibu wa mamlaka za nchi hiyo.
Wanakijiji walikuta miiili ya wasichaa hao wenye umri wa miaka 14 na 15 ikiwa inaning’inia katika mti wa maembe saa chache baada ya kupotea nyumbani katika kijiji cha Katra kilichopo kwenye jimbo la Utter Pradesh.
Wasichana hao walikuwa wamekwenda vichakani kuoga kutokana na kutokuwa na vyoo nyumbani kwao ambapo mamia ya wanakijiji wenye hasira walikusanyika katika eneo hilo la mti kwa siku nzima wakiandamana kushinikiza polisi kukabiliana na vitendo hivyo.
Social Plugin