Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

YULE MAMBA ALIYETISHIA MAISHA YA WATU HUKO KINONDONI HATIMAYE AUAWA LEO,TAZAMA PICHA HAPA

 Yule Mamba aliyekuwa akiishi kwenye makazi ya watu Kinondoni Block 41, jijini Dar es Salaam hatimaye leo May 4, 2014 ameuliwa kwa kupigwa na risasi zipatazo nne.

 Kwa mujibu wa shuhuda aliyekuwepo eneo la tukio alisema kuwa Mamba huyo amekuwa akiishi kwa muda mrefu licha ya Wananchi kutoa taarifa kwa mamlaka husika.

"Leo ameuawa Mamba ambaye alikuwa akitulaza kwa hofu maana alitokea kujichanganya kwenye makazi ya watu ndipo watu walipomshambulia na baadae ilibidi tupate msaada wa jirani yetu ambaye alikuwa na bastola  na kufanikiwa kumpiga risasi nne na kumuua. 
Mamba akiwa amewekwa juu ya gogo ili wananchi wamwangalie vizuri katika kituo cha Osterbay jijini Dar.
Mamba alikuwa amekomaa kukadiriwa anaumri wa miaka mitano...
Picha zote na EMMA Mdau wa Kajunason Blog akishirikiana na Erick Mgema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com