Walimu 97 katika shule ya msingi Nyankumbu na Mkombozi mjini Geita mkoani Geita wanatumia tundu moja la choo ambacho tena kiko kwenye nymba ya mwalimu huku wanafunzi wa shule hizo mbili 3563 wakitumia matundu 14 ya choo jambo ambalo limekuwa kero katika shule hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari hapo shuleni mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyankumbu Jasmin Ngume alisema kuwa awali ilikuwa shule moja baadaye imegawanywa na kuwepo Mkombozi shule ya msingi ambapo imeendelea kutumia tundu moja kwa walimu wote huku wanafunzi wakigawana matundu 7 kila shule.
Ameongeza kuwa kwa mujibu wa taratibu za wizara uwiano wa vyoo walimu wa kiume 4 hutumia tundu moja na walimu wa kike 3 hutumia tundu moja, na wanafunzi wakiume 3 hutumia tundu moja na wakike 4 hutumia tundu moja.
Aidha mwalimu huyo amesema kuwa kumekuwepo na sintofahamu ya walimu na wanafunzi namna ya kujisaidia kiasi kwamba wamekuwa wakienda kwenye nyumba za majirani na hata kuzuiliwa na kuambiwa kuwa shuleni si mna vyoo? jambo ambalo linawasababisha wakati mwingine kurudi nyumbani ili wakajisaidie huku muda wa kazi ukiwa bado anahitajika shuleni.
Uchunguzi wa mwandishi wa habari hizi umebaini kuwa shule hii ya muda mrefu awali ilikuwa ni ya ufundi na majengo ambayo yalikuwepo kipindi cha ufundi ni asilimia kubwa ndiyo yanayotumika kipindi kile huku kwa sasa shule ikipanuka na kuwa na wanafunzi wengi zaidi.
Baadhi ya wanafunzi walioongea na mwandishi wa habari hizi wamedai kuwa usumbufu wanaoupata unawasababishia kutosoma kwa raha na wakati mwingine wanahofia kula wakati wanakuwa na njaa kwa sababu itawalazimu waende
nyumbani.
Na Valence Robert wa Malunde1 blog -Geita