Imeripotiwa kuwa chui mwenye hasira na njaa aliingia majini na kupanda boti ya mvuvi aliyetajwa kwa jina la Shushil Manjhi huko Kolkata, India na kuondoka nae.
Taarifa zilizoripotiwa na vituo vya nchini India vinaeleza kuwa, mvuvi huyo alikuwa na watoto wake wawili (wa kike na wakiume) wakijaribu kutafuta kitoweo karibu na hifadhi ya taifa ya Sunderbans yenye wanyama wakali.
Mwanae wa kiume, Jyotish alieleza kwa njia ya simu kuwa chui huyo alirukia boti na kumkamata baba yake shingoni kwa upande wa nyuma na kuanza kumburuza akiondoka nae akielekea msituni.
“Alimrukia baba yangu kwa haraka mgogoni na kung’ata kwa nguvu kabla hajatokomea nae msituni.” Alieleza.
Mtoto huyo anaeleza kuwa baada ya chui huyo kumkamata baba yake, yeye na mdogo wake walijaribu kumpiga na fimbo na visu walivyokuwa navyo lakini hakuweza kumuachia.
Tukio hilo linatoa picha ya maisha duni ya wananchi masikini wa eneo hilo ambao licha ya kuwa na hatari kubwa ya kuuawa na wanyama wakali, hali ngumu ya maisha huwasukuma kuingia msituni kusaka kitoweo au chochote licha ya kwamba ni kinyume cha sheria kufanya uvuvi katika eneo la hifadhi ya wanyama.
Inaelezwa kuwa samaki wanaopatikana katika hifadhi hiyo hunuliwa kwa pesa nyingi katika miji ya jirani na vijiviji vya eneo hilo.
Social Plugin