Jumla ya Ng’ombe kumi na Moja na mbuzi wanne wameuwa na kuliwa na mnyama simba katika matukio matatutofauti yaliyotokea katika Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi baada ya simba kuvamia katika vijiji vitatu
Kwa mujibu wa Diwani wa Kata ya Mtapenda Elieza Fyula tukio la kwanza lilitokea hapo Mei 28 majira ya usiku katika Kijiji cha Kabatini .
Katika tukio hilo Simba walivamia kwenye kijiji hicho na kuua na kula Ng’ombe watatu na mbuzi watano ambao walikuwa wako ndani ya zizi la kufugia mifugo .
Alisema siku iliyofuata ya tarehe 29 meimajira ya usiku simba hao walivamia katika Kitongoji cha Kambike kilichoko katika Kijiji cha Isinde na kuwauwa Ng’ombe watano mali ya mfugaji wa kitongoji hicho aitwaye Dirisha na kisha waliwala ng’ombe hao.
DiwaniFyula alieleza baada ya tukio hilo viongozi wa kitongoji walitoa taarifa kwa viongozi wa kata ambao waliwasiliana na Idara ya Wanyama Poli ambao waliwasili kijijini hapo na kuwaswaga simba hao wapatao watano.
Alisema siku iliyofuata simba hao walivamia tena kwenye kijiiji cha mkumbi na kisha waliuwa Ng’ombe wawili na kuwala
Na Walter Mguluchuma -Katavi