Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HAYA NDIYO MAGEREZA 12 TANZANIA YASIYO NA SIFA ZA KUTUMIWA NA BINADAMU

Wakati mamilioni ya fedha za Watanzania yakipotea kila mwaka kutokana na ufisadi na misamaha ya kodi, imebainika kuwa baadhi ya magereza nchini hayafai kutumiwa na wafungwa kutokana na kukosa sifa ukiwemo uchakavu wa majengo.

Ripoti ya utafiti uliofanywa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwenye magereza na vituo vya polisi 102 katika mikoa 12, inaeleza kuwa magereza 12 hayafai kutumiwa na binadamu.

Hali hiyo inaamanisha kwamba magereza hayo siyo tu ni hatari kwa wafungwa na mahabusu, bali pia kiwa watumishi wa Idara ya Magereza. 

Ripoti hiyo inaweka bayana kuwa magereza hayo yana hali mbaya kutokana na majengo yake kujengwa miaka mingi iliyopita, huku mengine yakikabiliwa na ukosefu wa mwanga wa kutosha.

Magereza yaliyotajwa kukosa sifa za kutumiwa na binadamu ni Rombo, Nzega, Geita, Ngudu, Kasungamile, Ukerewe, Mugumu, Musoma, Bunda, Ushora, Mang’ola na Bariadi.

via>>fichuotz blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com