Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezindua mfumo wa rada ya kisasa na yenye uwezo mkubwa ijulikanayo kama Qader.
Mfumo wa Rada ya Qader umezinduliwa na kuanza kutekeleza oparesheni leo asubuhi katika sherehe iliyohudhuriwa na Brigedia Jenerali Farzad Esmaili kamanda wa Kambi ya Jeshi la Anga la Iran ya Khatamul Anbiya (SAW).
Rada ya Qader ina uwezo wa kutekeleza oparesheni katika eneo lenye upana wa kilomita 1100 na umbali wa juu wa kilomita 300.
Rada hiyo iliwahi kufanyiwa majaribio huko nyuma na sasa imewekwa katika maeneo mabli mbali ya Iran kulinda anga ya Jamhuri ya Kiislamu.
Jarida la kijeshi la Kizayuni la 'Israel Defense' limekiri kuwa ustawi wa kiteknolojia na kijeshi wa Iran ni mkubwa zaidi kuliko nchi za Magharibi zinavyodhani.
Jarida hilo limeandika kuwa Rada ya Qader ni ya kisasa kabisa na kwamba ni thibitisho la uwezo mkubwa wa Iran katika teknolojia ya kijeshi.
Rada ya Qader imetengenezwa katika Kituo cha Jihadi ya Kujitegemea ya Kitengo cha Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.
Rada hiyo ina uwezo wa kuainisha maeneo ya kulengwa angani mbali na kutambua ndege za adui ambazo hazionekani kwenye rada nyinginezo.
Aidha inaweza kutambua maeneo yanakorushwa makombora ya cruise na balistiki.
Hali kadhalika rada hiyo inaweza kutambua satalaiti zilizo katika anga za karibu na ina uwezo wa kufanya kazi katika mazingira yote ya hali ya hewa na uwezo wa kukabiliana na adui katika vita vya kielektroniki.
Social Plugin