Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAMA MTOTO WA BOKSI,SAFARI HII AFRIKA KUSINI,BABA AFUNGA MINYORORO WATOTO WAKE KWA MIAKA 8

Baba ya watoto hao anasema kuwa alikuwa anawalinda wanawe kwa kuwafunga kwa minyororo

Mwanamume mmoja wa Afrika Kusini aliyewafungia wanawe kwa minyororo katika chumba kimoja kwa miaka minane, amezuiliwa na polisi nchini humo.
Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 50, alifikishwa mahakamani mjini Alexandra, mtaa ambao uko Kaskazini mwa Johannesburg,kwa kosa la kutowalea wanawe vyema.

Watoto hao wenye umri wa miaka 14, 18 na 24, wote walikuwa na majeraha kwenye mikono yao na miguu.

Polisi wanasema kuwa watoto hao walipatikana baada ya mmoja wao mwenye umri wa miaka 24 ambaye pia ni mlemavu wa akili kutoroka.

Baba ya watoto hao alisema kuwa aliwafungia wanawe kwa usalama wao.

Polisi walikuwa na wakati mgumu kuwazuia wakazi waliojawa na gadhabu wakitaka kumshambulia mwanamume huyo na mkewe baada ya watoto wao kupatikana katika chumba hicho.

Majirani walitaja mazingira katika chumba hicho kama ya kusikitisha.
via>>bbc

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com