Mkazi wa kitongoji cha Budushi, Kata Mwendakulima, wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Antony Joseph 25- 26 amefariki dunia mchana wa leo baada ya kujitupia kwenye kisima cha maji akiwakimbia askari wa Jeshi la Polisi
Mwenyekiti wa kitongoji cha Budushi Zainab Kazi amesema Tukio hlo limetokea mchana wa leo baada ya Joseph kukamatwa kwa tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya utapeli, kwenye mtego ulioandaliwa eneo la benki ya NMB mjini Kahama.
Kazi amesema, Kijana huyo alituhumiwa kuwatapeli vijana wa kijiji cha Lugunga mkoani Geita ambao walifika katika kituo cha polisi Kahama kutoa taarifa ndipo mtego ulipoandaliwa na kufanikiwa kukamatwa.
Amesema Joseph aliwadanganya vijana hao kwamba ni mfanyakazi wa Benki ya Nmb kahama ambapo aliwaambia wampe hela ili awasaidie kuwafungulia Akaunti na kuwatafutia kazi mjini humo.
Kufuatia utapeli huo vijana hao waliweka mtego kwa kumpigia Simu kwa lengo la kumpa fedha zingine ndipo alipokamatwa na kuamriwa kwenda kwake ili kufanyiwa upekuzi nyumbani kwake.
Baada ya kuwa amefikishwa nyumbani kwake Mwendakulima akiwa chini ya ulinzi alimtishia kumpiga askari ndipo alipopata mwanya wa kukimbia na kujitupia kisimani.
Juhudi za kumwokoa zilifanyika ambapo walimtupia kamba ili atoke huku naye akikataa kutumia kamba hiyo kujiokoa hadi alipopoteza maisha kabla ya Kikosi cha zima Moto kufika eneo hilo na kumwopoa akiwa amefariki.
Social Plugin