KIJANA AUAWA BAADA YA KUVAMIA NYUMBA NA KUMCHARANGA MAPANGA MWANAMKE


Bi.Monica Lutonja akiwa anauguza majeraha yake katika hospitali ya wilaya ya Geita jana baada ya kukatwa na mapangwa .Picha na Valence Robert- Malunde1 blog-Geita.
Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Jumanne Joel(25-30) ameuawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kumvamia Monica Lutonja(32)  wa kijiji cha Nyankumbu katika kata ya Kalangalala mjini Geita .
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana ambapo inadaiwa kuwa watu watatu akiwemo marehemu walienda kwa mama huyo na kugonga hodi wakidai kuwa wao na rafiki wa kaka yake ambaye ni Bunegezi.

Baada ya Monica Lutonja kufungua walianza kumkatakata mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake hadi kupoteza fahamu.
Hata hivyo kelele za mama huyo zilisababisha majirani kutoka na kuanza kuwasaka baada ya kuwa wamekimbia na hatimaye wakamkamata mmoja na wakaanza kumpiga hadi kumuua.
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Joseph Konyo amethibisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa  watuhumiwa wengine wawili bado wanatafutwa na jeshi la polisi kwa ajili ya kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Na Valence Robert-Malunde1 Blog- Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post