Mwakifwamba na Dotnana wakiwa wamezama katika neno.
Mwakifwamba (wa pili kushoto) akiwa katika nguvu ya maombi.
Simon Mwakifwamba, Bahati Bukuku na Dotnata wakicheza wimbo wa Dunia Haina Huruma ulioimbwa na Bahati Bukuku.
Moja ya mabango yaliyokuwa kanisani.
Huyu ni Mchungaji Mbeyela ambaye ni mume wa mwibaji Upendo Nkone.
Kijana mpiga ngoma (drums) wa kundi la kwaya akifanya kazi yake kwa ufasaha.
‘’MATESO basi, damu ya Yesu yatosha’’. Hiyo ni kaulimbiu ya leo iliyotolewa katika Kanisa la Nchi ya Ahadi lililopo Sinza-Kamanyola jijini Dar, chini ya Mchungaji Kiongozi Harris Kapiga, wakati wa maombi maalumu kwa ajili ya wasanii wa Bongo Muvi ili kuvunja roho ya mauti juu ya tasnia hiyo ya filamu ambayo imewakumba wasanii wake.
Maombi hayo pia yalikuwa ni kuwaombea ulinzi wote waliomo na wanaotamani kuingia katika tasnia hiyo.
Maombi hayo yaliwakilishwa na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Saimon Mwakifwamba, wasanii na waimbaji Bahati Bukuku, Dotnata na wengineo.
(Na Gabriel Ng’osha, Shani Ramadhani na Chande Abdalah / GPL)
Social Plugin