Nyoka aliyekamatwa akiwa amekatwa katwa kabla ya kuteketezwa kwa moto.Picha na Ferdinand Shayo |
Nyoka akitembezwa baada ya kukamatwa katika kata ya Kiranyi jijini Arusha na kuuawa.Picha na Ferdinand Shayo |
nyoka akiuawa na wananchi baada ya kukatwakatwa |
Joka kubwa aina ya Chatu ameuawa wiki hii na Wananchi wenye hasira kali mtaa wa Azimio kata ya Kiranyi jijini Arusha baada ya kuonekana nyumbani kwa mtu
anayefahamika kwa jina la Joseph Magesa .
Aidha tukio hilo la kusimimua la la aina yake lilitokea jana majira ya saa 4 asubuhi ambapo inaelezwa kuwa joka huyo alipasua kioo cha nyumba na kutoka nje hali iliyompelekea mototo wa Magesa kuimbia nyumba hiyo pamoja
na mlinzi.
Baada ya Wananchi kupata taarifa za kuonekana kwa joka hilo nyumbani kwa magesa walifika nyumbani hapo na kumkuta nyoka huyo mkubwa akiwa anatambaa kuelekea nje ya geti ndipo alipojitokeza kijana mmoja ambaye
jina lake halikufahamika mara moja na kumvuta nyoka huyo kwa kutumia vitambaa alivyokuwa amefungiwa kwenye mkia.
George Enock ni mkazi wa eneo hilo ameeleza kuwa baada ya nyoka huyo kukamatwa alitembezwa mtaani mpaka majira ya saa 7 mchana ambapo alikatwa katwa na mapanga vipande baada ya hapo akateketezwa kwa moto.
Mkazi huyo anaeleza kuwa nyoka huyo alikuwa na ukumbwa zaidi ya futi 4alifikishwa nye ya Kanisa la Katoliki la St.Monica ambapo kila mwananchi kwa imani yake alifanya sala ,maombi na dua huku wengi wao wakimuhusisha
nyoka huyo na imani za kishirikina.
“Wako ambao walichukua vipande kadhaa vya nyoka huyo na kuondoka navyo pengine ni katika hali ya kuhakikisha kuwa joka huyo harejei tena kwa kuhofia kuwa angeweza kuhatarisha maisha ya watu” Alisema George.
Emanuel Sadick mkazi wa eneo hilo alisema kuwa nyoka huyo alikuwa amefungwa vitambaa vitatu vya rangi nyeusi,nyeupe na nyekundu ambavyo vilikua na
maandishi ambayo yalidaiwa kuwa ni ya lugha ya kiarabu .
Huenda nyoka huyo akawa anatumika kwenye mambo ya kishirikina mathalani umletea utajiri huyu bwana huwezi kujua tumehatarisha mtaji wa mtu.
Imeelezwa kuwa baada ya kukamatwa kwa nyoka huyo mwenye nyumba Magesa alipigiwa Simu na kuelezwa juu ya nyoka huyo na kuwataka wasimwue lakini hilo lakikuzuia hasira za wananchi ambao waliamua kumkata kata vipande nakumteketeza.
Naye Kiongozi mmoja wa Kanisa Katoliki la St.Monica lililoko jirani na Magesa ,kiongozi huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe amesema kuwa mtu huyo hana tabia ya kushiriki katika masuala ya kiroho (kanisa).
Viongozi wa kanisa waliwahi kumtembelea ili kumuomba awe anashiriki lakinijambo hilo halikufanikiwa.
“Watoto wake pekee ndio huwa wanafika kanisana na wakati mwingine huja kucheza na wenzao hapa kanisani lakini Magesa hajawahi kufika kabisa hapa kanisani licha ya kuwa ni Mkristu” Alisema kiongozi huyo.
Kwa upande wake Mchungaji Samweli Bonke wa kanisa la Wonders of Christ lilopo Sakina jijini hapa amedai kuwa mmliki wa nyoka huyo aliwahi kuishi mkoa wa Kigoma katika nyumba ya kupanga baada ya kuhama nyoka huyo
aligundulika kubaki kwenye hicho chumba lakini baadae alirudi na kumchukua.
Mchungaji huyo alisema kuwa Nyoka huyo ambaye aligundulika mwishoni mwa mwaka jana akiwa Kigoma na kujulikana kwa jina la Mtoto,baada ya Mwenye
nyoka kuhamia Arusha ambapo walipata taarifa na kufanya maombi na kufunga na kufanya maombi kwa muda wa siku 7 .
“Nikiwa Kigoma alikuja mtu mmoja na kuniomba nikaifanyie nyumba yake maombi baada ya kumuona nyoka huyo ambaye baadae aliondoshwa tukaomba ,leo
nashangaa kusikia ameuawa sisi tunaweza kusema maombi yetu yamejibiwa”Alisema Mchungaji huyo.
Naomi Molel ambaye ni shuhuda wa tukio hilo alisema kuwa nyoka huyo alikua mkubwa kiasi cha kutisha na kuwashangaza wakazi wa eneo hilo ambao walibaki
midomo wazi baada ya kumuona nyoka huyo.
Wakizungumza kwa Nyakati tofauti Amina Rajab na Fatuma Hussein wameeleza kuwa tukio hilo limewashtua wengi na kuzua gumzo katika eneo hilo .
Nyoka huyo anadaiwa kuwa na uwezo wa kummeza mtoto mdogo na iwapo angeendelea kuwepo pengine angehatarisha maisha ya wengi.
John Ibrahimu ,ambaye alishiriki katika kumtoa nyoka huyo nyumbani kwa Magesa hadi kumteketeza alifafanua kuwa nyoka huyo alivunja kioo cha nyumba na kutoka nje ambapo kupata taarifa walifika na kijana mmoja ambaye
walichukua kwa kumburuta hadi nje ya kanisa .
Mlinzi wa nyumba alikimbia pamoja na mtoto wa Magesa ,hata hivyo nyoka huyo alikua hana madhara maana tuliweza kumbeba na hakutudhuru ,kama nilivyotangulia kusema nyoka huyo anahusishwa na imani za kishirikina.
Wako wanaoamini kuwa kuna nyoka mwingine aliyesalia baada ya huyo mmoja kuuawa ambaye wanamwita mtoto,suala hilo bado linazua hofu miongoni mwa
wananchi.
Ziko tetesi za Mwenye nyumba Magesa kuwachukulia hatua wale wote ambao wamehusika katika kumkamata nyoka huyo na kumwua ,madai ambayo bado awajathibitishwa kwani alipotafutwa Magesa aongelee suala hilo hakuwepo
nyumbani kwake inadaiwa yuko jijini Dar es Slaam.
Na Victor Amath
Social Plugin