Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Makubwa haya!! MAITI YAKATWA MIGUU ILI IENEE KWENYE JENEZA,YADAIWA MIGUU YA MAREHEMU ILIKUWA MIREFU KUPINDUKIA

Miguu ya maiti inasemekana ilikuwa ndefu sana na kukwaza waandalizi wa mazishi

Mwandalizi mmoja wa mazishi nchini Afrika Kusini,anayedaiwa kuwaagiza wafanyakazi wake kuikata miguu ya maiti moja aliyodai kuwa ndefu sana alifikishwa mahakamani Ijumaa.

Ronel Mostert anayemiliki chumba cha kuhifadhi maiti ambacho pia huendesha shughuli za mazishi, alitoa amri hiyo kwa lengo la kuhakikisha kuwa maiti hiyo ingetosha katika jeneza.

Anakabiliwa na kosa la kumkata miguu maiti.

Mfanyakazi mmoja aliiambia mahakama kuwa Ronel alimuagiza kuchukua kifaa kimoja cha kukata ili kuikata miguu hiyo ya marehemu na kwamba jambo hilo limekuwa likimsumbua sana kimawazo.

Mwili marehemu ulifukuliwa ili kusaidia katika uchunguzi wa polisi.
via>>bbc

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com