Tofauti na inavyoaminika na wengi kuwa mfumaniwaji huwa mpole, kibao kimebadilika, mfanyakazi wa ndani aliyejulikana kwa jina la Niachie amegeuka mbogo na kumchoma bisibisi bosi wake, Amina ‘Mama Zai’ aliyemfumania akiwa na mumewe aitwaye Amri.
Tukio hilo lilitokea juzi kati maeneo ya Mbagala jijini Dar es salaam ambako mama Zai alimwekea mtego mfanyakazi wake huyo wa ndani baada ya kubaini kuwa alikuwa akitembea na mumewe wakati yeye akiwa kazini.
Akizungumza na mwandishi wetu siku mbili kabla ya tukio, mama Zai alidai kuwa mumewe ana kawaida ya kufanya mapenzi na mfanyakazi wao wa ndani wakati yeye akiwa kazini hivyo akaandaa mtego ili kukomesha tabia hiyo.
Mama Zai alizidi kumwaga data kuwa, yeye ni nesi katika hospitali moja ya mtu binafsi iliyoko Jangwani jijini Dar hivyo akiwa zamu ya usiku, mumewe hutumia mwanya huo kubanjuka na hausigeli.
“Ananivizia nikitoka tu na akijua nimeshafika mbali, anaingia chumbani kwa hausigeli na kuvunja naye amri ya sita,” alidai mama huyo.
Mama huyo alisema ili kufanikisha zoezi la kumnasa mumewe, alijifanya anakwenda zamu ya usiku kisha akajifungia stoo ili aweze kufanya fumanizi matata.
Ilipofika saa tano usiku, baba Zai aliingia katika chumba cha mfanyakazi huyo kwa lengo la kungonoka naye . Baada ya kuona hivyo, mama Zai alivamia chumba hicho na purukushani ya nguvu ikaanza.
Katika harakati za kujinasua katika kipigo cha bosi wake, hausigeli huyo aliokota bisibisi na kumchoma mama mwenye nyumba shingoni kisha kutimua mbio huku mume naye akiingia mitini.
via>> Global publisher
Social Plugin