Maskini!! MWANAFUNZI DARASA LA KWANZA ALAZIMISHWA KULA KINYESI KISA KAJISAIDIA KARIBU NA KISIMA CHA MTU HUKO GEITA

Mwanafunzi (Jina tunalihifadhi)(8) wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Nyakabale wilayani hapa amelishwa kinyesi chake baada ya kukutwa anajisaidia kwenye kisima akiwa na wenzake wakitoka shuleni.
 
Kamanda wa polisi mkoani wa Geita Joseph Konyo amesema kuwa tukio hilo limetokea tarehe 11 mwezi huu majira ya saa 4 asubuhi ambapo mwanafunzi huyo akiwa na wenzake watatu wakitoka shule kufanya usafi ,walipofika eneo hilo mwanafunzi mwenzao alienda kujisaidia karibu na kisima hicho cha  Marco Maico.
 
Akielezea zaidi kuhusu tukio hilo kamanda Konyo amesema mara tu mwanafunzi huyo alipomaliza kujisaidia, Marco alipita na kukuta kinyesi hicho.

Mmiliki wa kisima hicho Marcp Maico alimwamuru azoe kinyesi chake  kwa mkono kinyesi hicho.

 Hata hivyo alipoenda kukitupa Marco akamwambia akile hadi kiishe.

Kutokana na  hofu ya kutaka kupigwa mwanafunzi huyo alilazimika kula  kinyesi chake huku wenzake wakimsubiri  na baada ya kumaliza alienda nyumbani na wenzake.
 
Baada ya kufika nyumbani mwanafunzi huyo alimwambia mama yake Agnes Lujaja(26) juu ya kilichotokea na mama yake akaenda kwa balozi wa nyumba kumi kutoa taarifa ambapo akampa barua ya kumpeleka zahanati ya Nyakabale kwa matibabu.

 Baadaye balozi huyo alitoa taarifa kwa Polisi na baada ya muda walifika kwenye eneo la tukio na kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo.

Na Valence Robert-Malunde1 blog- Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post