Nasrah Rashid (kulia) enzi za uhai wake. Kushoto aliyekaa ni baba yake mzazi Rashid Mvungi.
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa mtoto Nasrah Rashid (4) aliyekuwa akitibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuugua na kupata ulemavu kwa kufungiwa kwenye boksi miaka minne amefariki dunia.
Nasrah alifichwa kwenye boksi na mama yake mkubwa aitwaye Mariamu Said mkazi wa Kiwanja cha Ndege, Morogoro tangu akiwa na miezi tisa baada ya mama yake mzazi kufariki.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU NASRAH MAHALI PEMA PEPONI .AMINA.
Social Plugin