|
Hapa ni katika kijiji cha Shilabela kata ya Pandagichiza halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ambako leo kumefanyika maadhimisho ya siku ya mazingira duniani katika mkoa wa Shinyanga.Aliyesimama ni mgeni rasmi katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Anselm Tarimo akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Shilabela katika maadhimisho hayo ambapo pamoja na mambo mengine aliupongeza uongozi wa kampuni ya Uchimbaji madini ya Dhahabu ya African Barrick (ABG)unaomiliki migodi ya Buzwagi na Bulyang'hulu katika mkoa wa Shinyanga kwa kuwa mstari wa mbele katika kutunza mazingira.
Aidha aliwataka wananachi katika mkoa wa Shinyanga hususani wilaya ya Shinyanga kubadilika na kujenga vyoo majumbani tofauti na ilivyo sasa kwani ni watu wachache wana vyoo kwenye kaya zao mfano katika kijiji cha Shilabela. Katika maadhimisho hayo siku ya mazingira duniani,African Barrick mkoa wa Shinyanga ilifanya maonesho kuhusu shughuli inazofanya kuhusiana na utunzaji wa mazingira. |
|
Ndani ya Banda la maonesho-Kulia ni afisa Mazingira wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi bi Naziel Eliakimu akitoa maelezo kwa mgeni rasmi katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Anselm Tarimo(wa kwanza kushoto) kuhusu shughuli zinazofanywa na kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya African Barrick kuhusu utunzaji wa mazingira.Eliakimu alisema ABG inafanya shughuli nyingi kama vile kudhibiti udongo,wanyama na mimea,hali ya hewa,maji,kemikali na taka.
|
Afisa Mazingira wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi bi Naziel Eliakimu alisema pia ABG huwa inatoa elimu kwa wananchi na wafanyakazi wake kuhusu utunzaji wa mazingira na kuwajibika kwa jamii.Nyuma yake ni afisa mazingira kutoka mgodi wa Bulyang'hulu bi Sibilina Mvungi.Kifaa unachokiona hapo mbele kushoto ni miongoni mwa vifaa vinavyotumiwa na ABG kukamatia nyoka katika maeneo ya mgodi
|
Aliyeshikilia kipaza sauti(Mic) pia ni afisa mazingira kutoka mgodi wa Buzwagi bwana Tunzo Msuya akizungumza wakati maonesho yao kuhusu mambo ya mazingira ambapo alisema ili kuwa rafiki wa mazingira wamekuwa wakielimisha jamii,vikundi na shule mbali mbali kuhusu umuhimu utunzaji wa mazingira |
|
Akiyeshikilia kipaza sauti ni afisa Mahusiano wa mgodi wa Buzwagi bwana Moses Msofe ambaye alisema kampuni ya ABG imekuwa mstari wa mbele katika kupiga vita uchafuzi wa mazingira |
|
Maonesho yanaendelea- Aliyesimama ni afisa mahusiano mgodi wa Bulyang'hulu bi Zuwena Senkondo alisema ABG imekuwa ikihamasisha wananchi kupanda miti,kufuga nyuki na kuunda vikundi mbalimbali vya utunzaji wa mazingira hayo yote ni katika kukabiliana na uchafuzi wa mazingira |
|
Wananchi mbalimbali wakiwa katika kibanda cha maonesho cha ABG ambao walikuja na miche ya miti ya matunda kama vile maembe,mapapai na maparachichi na kuwagawia wananchi wa kijiji cha Shilabela kata ya Pandagichiza wilaya ya Shinyanga ambako kimkoa maadhimisho ya siku ya mazingira duniani imefanyika |
|
Ndani ya banda la maonesho-Akiyeshikilia kipaza sauti ni afisa Mahusiano wa mgodi wa Buzwagi bwana Moses Msofe akizungumzia shughuli ya ufugaji nyuki inayofanywa na kikundi cha kata ya Mwendakulima wilayani Kahama kupitia mgodi wa Buzwagi.Katikati ni katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Anselm Tarimo akiwa ameshikilia asali aliyopewa na ABG kama zawadi,kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku akiwa ameshikilia asali aliyopewa na ABG kama zawadi |
|
Afisa mazingira kutoka mgodi wa Buzwagi bwana Tunzo Msuya akikabidhi mti wa matunda kwa mgeni rasmi katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Anselm Tarimo kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira duniani mkoa wa Shinyanga.Kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick wanajishughulisha pia na uzalishaji wa miti |
|
Afisa mahusiano mgodi wa Bulyang'hulu bi Zuwena Senkondo akikabidhi mche wa mti kwa katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga ndugu Boniface Chambi |
|
Afisa mahusiano mgodi wa Bulyanhulu bi Zuwena Senkondo akionesha bidhaa kama vile vikapu,pochi ,mifuko na kofia zinazotengezwa na kikundi cha Tupendane kilichopo katika halmashauri ya Msalala kilichoanzishwa Oktoba 4,2013 kikiwa na wanachama wanne na sasa 33.Kikundi hicho hutumia mifuko laini iliyotumika(rambo laini) kutengeneza bidhaa hizo.Hawa ni rafiki wa mazingira kwani badala ya kutupa mifuko hiyo,sasa wanatengeneza bidhaa ambazo zinawaingizia kipato,mradi ambao umeanzishwa na ABG kupitia mgodi wake wa Bulyanhulu.Wa pili kushoto ni katibu wa kikundi cha Msalala bi Jenifa Robert,Wa tatu ni mmoja wa wanakikundi cha wafuga nyuki cha Mwendakulima bi Rehema Juma |
|
Mgeni rasmi ambaye ni katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Anselm Tarimo akizungumza alipotembelea banda la maonesho la ABG ambapo aliwapongeza kwa rafiki wa mazingira na kuyataka makampuni mengine kuiga mfano wa African Barrick katika kutunza mazingira na kuwataka wananchi waliopata bahati ya kupewa miche ya miti kuitunza vizuri |
|
Baada ya Maonesho-Jeshi la jadi sungusungu maarufu kama Wasalama katika kijiji cha Shilabela wakitoa burudani wakati wa maadhimisho ya siku ya mazingira duniani katika mkoa wa Shinyanga |
|
Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinajiri |
|
Afisa maliasili na mazingira mkoa wa Shinyanga ndugu Bilie Edimot ambaye pia ni mratibu wa maadhimisho ya siku ya mazingira duniani,akizungumza katika maadhimisho hayo ambapo alisema wilaya iliyoshinda na kupewa tuzo ya hifadhi ya mazingira mkoa wa Shinyanga mwaka huu ni halmashauri ya wilaya ya Kishapu na kuhusu usafi wa mazingira ni halmashauri ya mji Kahama ikifuatiwa na halmashauri ya wilaya ya Kishapu huku wilaya iliyofanya vibaya kuliko zote ni wilaya ya Shinyanga ambayo leo ilikuwa mwenyeji wa maadhimisho ya siku ya mazingira duniani katika mkoa wa Shinyanga |
|
Afisa maliasili na mazingira mkoa wa Shinyanga ndugu Bilie Edimot aliongeza kuwa mshindi wa tuzo ya uhifadhi wa mazingira katika ngazi ya mkoa mzima wa Shinyanga mwaka huu imechukuliwa na bwana Paul Kadonya kutoka kijiji cha Nyandekwa,kata ya Nyandekwa halmashauri ya mji Kahama.Kijiji kilichofanya vizuri kuliko vyote mkoa mzima ni Kijiji cha Buganzo kata ya Ntobo halmashauri ya Msalala na kwa upande wa kata ni kata ya Ntobo mkoa mzima wa Shinyanga |
|
Jukwaa kuu wakimsikiza afisa maliasili na mazingira mkoa wa Shinyanga ambaye pia alisema washindi wa hifadhi ya mazingira mwaka huu katika ngazi ya shule ya elimu ya msingi ni shule ya msingi Ufala iliyopo kata ya Kilago halmashauri ya mji Kahama,na upande wa shule za sekondari ni shule ya Anderlek Ridges iliyopo katika kijiji cha Nyakato,kata ya Mhongolo halmashauri ya mji Kahama. |
|
Afisa Mahusiano wa mgodi wa Buzwagi bwana Moses Msofe (kwa niaba ya African Barrick)akipokea zawadi ya cheti kutoka kwa katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Ndugu Anselm Tarimo kama wadau muhumu wa mazingira katika mkoa wa Shinyanga |
|
Afisa afya wa mkoa wa Shinyanga Neema Simba akipokea zawadi kwa niaba ya Paul Kadonya ambaye ni mshindi wa tuzo ya uhifadhi wa mazingira ngazi ya kaya ambaye ni mkazi wa kijiji cha Nyandekwa kata ya Nyandekwa halmashauri ya mji Kahama ambaye hakuhudhuria maadhimisho hayo. |
|
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku akiwasalimia wakazi wa kijiji cha Shilabela kata ya Pandagichiza wilaya ya Shinyanga ambapo alieleza kufurahia ushindi wa wilaya yake mwaka huu katika kuhifadhi mazingira.Kauli mbiu ya siku ya mazingira duniani mwaka huu ni "Tunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi" Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga |
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com