Hatimaye Mtoto Nasra Mvungi aliyefariki Juni mosi mwaka huu kufuatia kuishi katika mateso makubwa kutoka kwa mama yake mkubwa baada ya mama yake kufariki na kuishi katika boksi bila huduma muhimu anazostahili kupatiwa binadamu hasa mtoto mdogo mwenye umri wa mwaka mmoja amezikwa kwa heshima zote na wakazi wa Morogoro wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Joel Nkaya Bendera, Mbunge wa Morogoro mjini, Abdulaziz Abood na mfanyabiashara wa mabasi na vituo vya mafuta mkoani Morogoro Al Saed Omary.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, ametaka vyombo vya sheria Mahaka, kutoa hukumu inayowastahili waliohusika kwa mateso na kupelekea kifo cha Nasra.
Waombolezaji wakiwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, kuaga mwili wa mtoto Nasra Mvungi.
Mfanyabiashara, Al Saed Omary aliyefanikisha kuleta mwili wa marehemu Nasra kutoka Dar es Salaam.
Waombolezaji wakiingia katika mabasi ya Abood, kwenda katika maziko.
Mazishi ya mtoto Nasra yakiendelea makaburi ya Kola mkoani Morogoro.
Mbunge Abdulaziz Abood akiweka udongo katika kaburi la marehemu Nasra na kuahidi kumfanyia hitma baada ya siku 40 tangu kuzikwa kwake.
Mfanyabiashara Al Saed Omar nae akiweka udongo katika kaburi la marehemu.
RASHID Mvungi, baba mzazi wa mtoto Nasra (4), aliyefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, alikolazwa kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimkabili yanayosadikiwa kuchochewa na mateso aliyoyapata alipokuwa akiishi kwenye boksi kwa takribani miaka minne, ameshindwa kumzika mwanae katika makaburi ya Kola, Manispaa ya Morogoro.
Kushindwa kwake kuhudhuria kuweka undogo katika kaburi la mwanae ni baada ya kuzuiwa na Polisi kwenda makaburini kwa madai ya kumwepusha na hatari ya hasira za wananchi kwa unyama waliomfanyia Narsa na walezi wake wawili.
Baba mzazi huyo, licha ya awali kushiriki kwenda Jijini Dar es Salaaam kuuchukua mwili wa mwanaye pamoja na viongozi wa Idara ya Ustawi wa Jamii Mkoa na Polisi kitengo cha Dawati la Jinsia, pia alikuwepo uwanja wa Jamhuri wa Mjini hapa kushiriki shughuli za kuangwa kwa mwili wa mtoto huyo.
Mvungi alikuwa ameketi mstari wa mbele ya jeneza la mwanaye wakati wote wa kutolewa nasaha mbalimbali za viongozi wa Serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa, Joel Bendera na wale wa dini wakiendesha sala ya kabla ya mwili kuondolewa kwenda msikitini kusaliwa.
Hata hivyo mara baada ya kumalizika shughuli hiyo Mvungi alichukuliwa na Askari Polisi wa kitengo cha Upelelezi Mkoa.
Akihojiwa na Mwandishi, eneo la Makaburi ya Kola, juu ya kutoonekana kwa baba mzazi wa marehemu, Narsa, Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa, Kibona, alisema kuwa, isingekuwa jambo la busara kuruhusu Mvungi ashiriki mazishi makaburini kutokana na kuhofia hasira za wananchi.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mkoa, kuwa Mvungi aliondolewa uwanjani hapo kwa ajili ya kulinda usalama wake mara baada ya kumalizika kwa shughuli za kuangwa kwa mwanaye.
NA John Nditi, Morogoro