Mfanyabiashara mmoja tajiri raia wa China amekutwa na hatia ya kula Chui watatu ambapo amekiri kufanya kitendo hicho.
Mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina moja la Xu kutoka Kusini Magharibi mwa Jimbo la Guangxi, anadaiwa kuipenda ladha ya Chui hao pamoja na damu.
Mwanaume hao alifanikiwa kununua Chui hao walioingizwa kimagendo na kundi la marafiki zake kutoka nje ya China.
Walikamatwa na polisi waliozingira sherehe yao ya kuchoma nyama ya Chui waliyoiandaa kuonyesha utajiri wao.
Nchini China, Chui wanachukuliwa kama alama ya Ujasiri na Nguvu ambapo waganga wa kimila hutumia baadhi ya viungo vya miili yao kwa ajili ya dawa za magonjwa mbalimbali kama kuumwa mifupa na kuongeza uwezo wa macho kuona.
Waendesha mashtaka katika mji wa Qinzhou wanasema kuwa Bw. Xu ana appetite ya haraka ya kula uume wa Chui pamoja na kunywa damu yao.