Msaada!! TAZAMA PICHA MGONJWA ALIYEOZA MAKALIO KISHA KUTIMULIWA BUGANDO,TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI
Wednesday, June 11, 2014
Hali halisi ya makalio ya Joseph Luhogola
(38),mkazi wa Kitongoji cha Nyabugera,Kijiji cha Mganza Wilaya ya Chato katika
Mkoa wa Geita ambapo Hospitali ya rufaa ya Bugando ya Jijini Mwanza baada ya
kudaiwa kumtimua Mgonjwa wake ambaye ameozea Wodini hapo na sasa anaendelea
kuoza akiwa nyumbani kwa mganga wa tiba za asili.
Joseph Luhogola (38),mkazi wa Kitongoji cha Nyabugera,Kijiji cha Mganza Wilaya ya Chato katika Mkoa wa Geita akiwa amelala nyumbani kwa mganga wa tiba za asili Paul Chasama ambaye
ni mtaalamu wa tiba za jadi kwa kuunga mifupa na kurudisha viungo
vya mwili vilivyochengana ambaye ni mkazi wa Kitongoji cha Elimu,katika kijiji
cha Nyankumbu Wilayani Geita amedai kuwa,kutokana na uzoefu kwenye kazi hiyo
anao uhakika wa asilimia mia kwamba Luhogola atapona.
Baadhi ya watu wamedai
iwapo mganga Chasama atafanikiwa kumponya kijana huyo aliyeoza makalio yake
kama unavyoona pichani basi watalazimika kuwaondoa wagonjwa wao hospitali na
kuwapeleka kwake.Picha zote na Victor Bariety-Geita
Kama umeguswa na habari
hii ya kusikitisha wasiliana na mwandishi wa Malunde1 Blog mkoani Geita ndugu Victor Bariety kwa simu namba 0763 681 747 kwa ajili ya msaada kwa
mgonjwa aliyeoza makalio ndugu Joseph Luhogola
Social Plugin