Taarifa kutoka Colorado, Marekani zinaeleza kuwa Msichana mwenye umri wa miaka 19, anafahamika kwa jina la Isabella Yun-Mi Guzman ambaye alimchoma mama yake visu mara 151 ameachiwa huru.
Mahakama imemuachia huru Isabella baada ya kubaini kuwa ni mgonjwa wa akili na kwamba wakati anatekeleza tukio hilo hakuwa katika hali ya kawaida kiakili hivyo kwa mujibu wa sheria hana hatia.
Mahakama imeamuru msichana huyo kupelekwa katika hospitali ya wagonjwa wenye matatizo ya akili kwa ajili ya kupata matibabu badala ya kumpeleka jela.
Kwa mujibu wa ripoti zilizofikishwa mahakamani hapo na polisi, Issabella alimchoma mama yake visu mara 151 (Mara 35 usoni, mara 51 shingoni, na mara 65 katika sehemu nyingine za mwili.
Msichana huyo amepelekwa Colorado Mental Health Institute.
Social Plugin