WAKATI Kesi ya Msusa Omary Masusa (40) aliyefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Wilaya Ya Tunduru kujibu tuhuma za kumbaka na kumlawiti Mtoto wa miaka 7
Mtoto huyo (Jina linahifadhiwa na mtandao huu) amebakwa tena na mhusika kufikishwa katika mahakama hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa za tukio hilo mtuhumiwa wa pili amefahamika kwa jina la Said All Nasoro (31) ambaye kwa sasa anakabiliwa na Shauri la kubaka namba 39/2014 ambapo anadaiwa kuwa alifanikisha kutekeleza unyama huo baada ya kumdanganya mtoto huyo kuwa angemnunulia Chakula na pipi.
Akimsomea shtaka hilo mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Felix Nyalanda, mwendesha mashitaka mkaguzi msaidizi wa polisi Inspekta Songelaeli Jwagu alisema kuwa mtuhumiwa huyo kwa makusudi alitekeleza unyama huo mei 25 mwaka huu majira ya mchana wakati wazazi wa mtoto huyo wakiwa shambani.
Inspekita Jwagu aliendelea kufafanua kuwa katika tukio hilo mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo kinyume cha vifungu vya sharia namba 130 kifungu kidogo cha (1) na (2) na namba 131 vya sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Alisema katika Tukio hilo Kijana huyo kwa kukusudia alimchukua hadi nyumbani kwake na kumvamia na kumbaka mtoto huyo ambaye ni mlemavu wa akili aliyemtaja kwa jina ila blog hii inalihifadhi.
Mtuhumiwa huyo alikana kufanya kosa hilo, na amepelekwa mahabusu ya gereza la Wilaya ya Tunduru baada ya kukosa mtu wa kumdhamini.
Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka huyo uchunguzi wa kesi hiyo bado haujakamilika kesi italetwa tena Juni 17 mwaka huu katika mahakama hiyo kwa ajili ya kutajwa
AKizungumzia tukio hilo nje ya mahakama Mama mzazi wa mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya msingi Matemanga Bi.Halima Mtola alisema kuwa siku ya tukio yeye alikwenda msibani na kumuacha akiwa na mdogo wake na aliporudi majira uya saa 6. Usiku hakumkuta na ndipo akaanza kumtafuta hadi walipo mnasa akiwa ndani kwa mtuhumiwa.
Alisema katika tukio hilo waliwakuta wote wakiwa Uchi wa mnyama Nyumbani kwa mtuhumiwa majira ya saa 7. za usiku na walipoanza kupiga kelele za kuomba msaada mtuhumiwa aliruka ukuta na kukimbia.
Alisema kitu kinachowafanya watu hao kuendeleza unyama huo kwa mtoto wake huyo kinatokana na uonevu wa kijinsia huku wakiwa wanatumia udhaifu wa mapungufu ya ugonjwa wa akili anaougua kwa muda mrefu.
Aidha akiongea kwa uchungu Mama huyo aliviomba vyombo vya sheria kuwachukulia hatua kali watu hao kutokana na kutenda unyama huo kwa mtoto huyo mwenye umri mdogo.
Na Steven Augustino- Tunduru
Social Plugin