Mwanafunzi wa chuo cha kilimo cha Maluku mwaka wa kwanza kilichopo Bukoba Joseph Futi(28) amekutwa amejinyonga hadi kufa katika mtaa wa Shilabela kata ya Kalangalala mjini Geita.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo ambapo imeelezwa kuwa mwanafunzi huyo alikuwa amekuja likizo nyumbani kwao.
Kaka wa marehemu Marco Samweli amesema kuwa mdogo wake alifika ijumaa kutoka chuoni baada ya kufunga kwa likizo na alipokuwa nyumbani siku ya jumamosi aliondoka akaenda mjini kuchaji laptop yake na yeye aliondoka kwenda kazini kwake.
"Nilipotoka kazini jioni sikumkuta nyumbani nikamuuliza mke wangu mdogo waangu yuko wapi akasema hajafika tangu aondoke asubuhi kupeleka laptop mjini baadaye majira ya saa 3 usiku nilianza kumpigia simu ili kutaka kujua yuko wapi",alieleza
"Simu yake iliita bila kupokelewa na hata nilipotuma ujumbe mfupi wa maneno haukujibiwa baada ya hapo nilikaa na kutulia hadi leo asubuhi nikapigiwa simu kuwa mdogo wangu amejinyonga hadi kufa kwa kamba kwenye mti",aliongeza
Afisa mtendaji wa kata ya kalangalala Hamad Hussen amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Kamanda wa polisi mkoani hapa Joseph Konyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa wanaendelea kuchunguza ili kubaini chanzo cha tukio hilo.
Na Valence Robert wa Malunde1 Blog -Geita
Social Plugin