Marehemu Fides Chale (1940 - 2014).
TGNP Mtandao tumepata pigo kubwa kwa kumpoteza mwanaharakati na Mwenyekiti wa kwanza wa shirika, aliyefariki Juni 2, 2014 Ubungo Msewe Dar es Salaam.
Fides Chale alikuwa ni mwalimu na kiongozi aliyegusa maisha ya wengi hapa Tanzania, Mwanaharakati mtetezi wa haki za wanawake, wasichana na makundi mengine yaliyoko pembezoni.
Dada Fides amekuwa mtu wa watu, mcheshi, mwenye upendo, utu, huruma, mpole, mwenye sura ya kutabasamu muda wote hata alipokuwa kwenye hali ya ugonjwa.
Tunapoombeleza kumpoteza dada yetu Fides Chale, tunasheherekea maisha yake mchango wake mkubwa jinsi alivyojitolea kwa hali na mali kulilea shirika tangu lilipoanza hadi mauti yalipomfika.
Fides Chale alishika uongozi TGNP wakati shirika likiwa changa, kuliwekea misingi imara na endelevu wa kiuongozi, kiutawala, na mfumo mzuri wa kubadilishana uongozi unaoendelea hadi leo.
Mipango ya mazishi inaendelea nyumbani Ubungo Msewe.
Alhamis 05/06/2014 ibada itafanyika katika Kanisa Katoliki Mt. Petro Osterbay na kufuatiwa na mazishi katika makaburi ya Kinondoni.
Imetolewa na; Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, TGNP Mtandao
Social Plugin