Mamlaka nchini Australia imetoa tahadhari dhidi ya matumizi ya charger aina ya USB feki au zilizo chini ya viwango huku zikiwa zimechomekwa kwenye umeme baada ya mwanamke mmoja kufariki dunia wakati akitumia charger ya aina hiyo kucharge simu yake iliyokuwa imechomekwa kwenye kompyuta yake ndogo.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 28 alikutwa amevaa headphones masikioni akiwa na kompyuta yake mikononi huku akiwa na majeraha ya kuungua kifuani na masikioni nyumbani kwake huko Gosford, Kaskazini mwa Sydney.
Polisi nchini humo bado wanafanya uchunguzi kujua mazingira ya kifo hicho lakini kitengo cha biashara kilichofuatilia suala hilo kimetahadharisha kuwa charger za simu zilizo chini ya viwango ni moja ya sababu kubwa.
Mwanamke huyo ambaye ripoti zinadai kuwa anatokea nchini Ufilipino na baadae kuwa raia wa Australia alivaa headphones zilizokuwa zimechomekwa kwenye kompyuta ndogo iliyokuwa imechomekwa kwenye socket ya umeme.
Social Plugin