Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWANAMKE AJITOA MHANGA,AVAMIA KAMBI YA JESHI

Rais Goodluck Jonathan
Mwanamke aliyejitolea mhanga alijiripua nje ya kambi ya jeshi, kaskazini-mashariki mwa Nigeria.
Wanajeshi wawili walijeruhiwa vibaya.


Aliripua bomu wakati akihojiwa na wanajeshi.Afisa wa jeshi aliiambia BBC kwamba mwanamke huyo aliyevaa hijabu, alikaribia kambi kwa piki-piki katika jimbo la Gombe.

Mwandishi wa BBC katika eneo hilo, anasema siyo kawaida kwa mwanamke kushambulia kwa kujitolea mhanga nchini Nigeria, na jimbo la Gombe limekuwa salama kwa jumla.
Hakuna kundi lilodai kufanya shambulio hilo.
Lakini kundi la Waislamu la Boko Haram, limekuwa likilenga makambi ya jeshi na polisi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com