June 05 2014 mchana kupitia mitandao mbalimbali Tanzania zilisambaa taarifa zikimuhusu mmiliki wa mojawapo ya nyumba maeneo ya Sakina jijini Arusha kwamba nyoka aliyekua akimfuga kwa siku nyingi na kuhusishwa na imani za kishirikina, ameuwawa na Wananchi.
Wananchi walimuua nyoka huyo na kisha kumkata kata vipande vipande ambapo baada ya hizi taarifa kusambaa mmiliki wa nyumba hii ameamua kufunguka ili kutoa maelezo yake ambayo anadai ndio ukweli wenyewe.
Mr.Joseph Paschal Magesa anasema, "Mimi kama mimi kwanza ni Mkristo safi na mzee wa kanisa na niliondoka nyumbani jana na mke wangu kutoka Arusha kuelekea Dar es salaam, sijui lolote kuhusiana na hicho kitu ila nilipofika maeneo ya Mwanga na Same nikapigiwa simu kwamba kuna nyoka huku ndani ya eneo la garden nyumbani, kuna vijana niliwaacha wawili pale nyumbani nikawaambia waambieni watu wawasaidie kumuua huyo nyoka"
"Wakamuita jirani yangu hapo ndipo naye akanipigia simu nikamwambia bwana wewe si una bunduki nisaidie kumuua huyo nyoka ila alivyokata simu nilijua ametekeleza kumbe aliondoka, baadaye napiga tena simu nauliza vipi naambiwa bado yupo na watu wamejaa nikawauliza kwani hao watu hawawezi kumuua mpaka bunduki wakasema wanaweza ndio baadae wakanambia wamemvuta mkia wamemuweka nje ya geti"
"Nikawauliza anavutika, asije akawa analeta shida wakasema anavutika, nikawaambia mpelekeni kanisani kwa sababu nyumbani kwangu ni jirani na kanisa ndio wakamvuta hadi kanisani wakammwagia maji ya baraka kisha wakamkatakata ndo ikawa mwisho wake hapo".
"Kusema kwamba nilikua nafuga kwamba huyu nyoka ni mtoto wangu wa kwanza….. sasa kama ni mtoto wangu wa kwanza si inamaana na mtoto wangu angekufa na yeye? mimi nasema namwachia Mungu tu…….. sijawahi kusikia Nyoka kuishi maeneo hayo toka nimeanza kuishi kwa karibu miaka 8, hata na mimi inanitatiza manake nimetumiwa picha Nyoka amefungwa kitambaa chenye maandishi mekundu kama ya kiarabuarabu hivi….."
"Taarifa kwamba Nyoka huyu amevunja kioo cha dirisha akiwa anatokea ndani ya nyumba, sio kweli…. haipo kabisa hiyo kitu eti kwamba ametokea ndani, hayo ni mambo ya watu tu… hicho kioo nilikivunja mimi wakati napanga mizigo ya ofisi yangu… sifahamu chochote kuhusu huyu Nyoka, Watanzania waniamini haya ninayosema ndio yanayotoka moyoni mwangu"
Social Plugin