Mrembo aliyeonekana kwenye picha inayodaiwa kutengenezwa kitaalam akiwa na mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapten John Komba, anasakwa kwa udi na uvumba....
Kusakwa kwa mwadada huyo anayedaiwa kuishi maeneo ya Kinondoni jijini Dar es salaam, kumekuja siku chache tangu mbunge huyo atoe taarifa kwamba hauhusiki na picha hizo na ana imani kwamba zimetengenezwa na wabaya wake....
Inaaminika kwamba kupatikana kwa mwanamke huyo kutategua kitendawili kuhusiana na tukio hilo.
Taarifa iliyotolewa na mbunge huyo ilisema kwamba picha hizo zimetengenezwa na maadui wake wa kisiasa na kwamba yeye siyo kiongozi wa hovyo hovyo namna hiyo....
Komba alisema kwamba anawakaribisha wataalamu wa picha na mitandao kuthibitisha ukweli wa picha hizo kama zinamhusu.
Mbunge huyo alihoji, iweje awe kwenye mapenzi kama picha hizo zinavyoonesha halafu awe na nguo zake zote huku msichana akiwa na kanga tu?
Kapteni Komba alisema kama taifa limefikia hatua ya kuchafuana sababu ya mitizamo tofauti ya kisiasa juu ya namna ya kuongoza taifa letu basi tumefika pabaya sana....
Alisema wale wote wanaomuamini kama kiongozi shupavu wasikatishwe tamaa na wachache wenye mawazo ya kitumwa ambao wanadhani wanaweza kummaliza kisiasa kwa kumtengenezea picha chafu kama hizo...
Katika hatua nyingine, wadau mbalimbali wameomba kusakwa kwa mtu aliyezitengeneza na kuzitoa picha hizo kwenye mitandao ya kijamii ili ahojiwe...
Wadau hao walisema, mtu huyo akipatikana na kuhojiwa ndipo itajulikana nini kilikuwa chanzo cha kufanya jambo hilo .
Social Plugin