Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Noma kweli kweli!! MREMBO ALIYEONEKANA KIMAHABA NA MHESHIMIWA JOHN KOMBA ASAKWA KWA UDI NA UVUMBA




Mrembo  aliyeonekana  kwenye  picha  inayodaiwa  kutengenezwa  kitaalam  akiwa  na  mbunge  wa  Mbinga  Magharibi, Kapten John Komba, anasakwa  kwa  udi  na  uvumba....

Kusakwa  kwa  mwadada  huyo  anayedaiwa  kuishi  maeneo  ya  Kinondoni  jijini  Dar  es salaam, kumekuja  siku  chache  tangu  mbunge  huyo  atoe  taarifa  kwamba  hauhusiki  na  picha  hizo  na  ana  imani  kwamba  zimetengenezwa  na  wabaya  wake....

Inaaminika  kwamba  kupatikana  kwa  mwanamke  huyo  kutategua  kitendawili  kuhusiana  na  tukio  hilo.

Taarifa  iliyotolewa  na  mbunge  huyo  ilisema  kwamba  picha  hizo  zimetengenezwa  na  maadui wake  wa  kisiasa  na  kwamba  yeye  siyo  kiongozi  wa  hovyo hovyo  namna   hiyo....

Komba  alisema  kwamba  anawakaribisha  wataalamu  wa  picha  na  mitandao  kuthibitisha   ukweli  wa  picha  hizo  kama  zinamhusu.

Mbunge  huyo  alihoji, iweje  awe  kwenye  mapenzi  kama  picha  hizo  zinavyoonesha  halafu  awe  na  nguo  zake  zote  huku  msichana  akiwa  na  kanga  tu?
Kapteni  Komba  alisema  kama  taifa  limefikia  hatua  ya  kuchafuana  sababu  ya  mitizamo  tofauti  ya  kisiasa  juu  ya  namna  ya  kuongoza  taifa  letu  basi  tumefika  pabaya  sana....

Alisema  wale  wote  wanaomuamini  kama  kiongozi  shupavu  wasikatishwe  tamaa  na  wachache  wenye  mawazo  ya  kitumwa  ambao  wanadhani  wanaweza  kummaliza  kisiasa  kwa  kumtengenezea  picha  chafu  kama  hizo...

Katika  hatua  nyingine, wadau  mbalimbali  wameomba  kusakwa  kwa  mtu  aliyezitengeneza  na   kuzitoa  picha  hizo  kwenye  mitandao  ya  kijamii  ili  ahojiwe...

Wadau  hao  walisema, mtu  huyo   akipatikana  na  kuhojiwa  ndipo  itajulikana  nini  kilikuwa  chanzo  cha  kufanya  jambo  hilo .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com