Ndege inayoendeshwa kwa kutumia nguvu ya jua ya Solar Impulse 2 aircraft ambayo ni ya pili katika mfululizo wa ndege za aina hiyo zinazotengenezwa nchini Uswizi leo imeanza safari yake ya kwanza kutoka katika kiwanja chake Magharibi mwa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa watengenezaji, Ndege hiyo ambayo kwa asilimia kubwa inategemea nguvu ya jua ilipaa angani kwa takribani saa mbili na dakika 15 na kufanikiwa kuruka umbali wa mita 2400.
Kabla ya kufanya majaribio ya toleo hilo la pili, marubani wa ndege hiyo André Borschberg na Bertrand Piccard walitumia muda mwingi katika toleo la kwanza la ndege kama hiyo iliyopaa Ulaya hadi Moroco na kupitia nchini Marekani mwaka 2010 kwa muda wa saa 26 bila kutua.
Baada ya muda mrefu wa majaribio na maandalizi, Watengenezaji hao na marubani wamefanikiwa kuirusha ndege ya pili leo kwa kutumia jua pekee ambapo ilitua saa mbili baadae.
Solar Impulse 2 ni kubwa zaidi ya ile ya kwanza lakini ina uzito mdogo ukilinganisha na baadhi ya magari.
Viti vya ndege hiyo vinaweza kulala ambapo sehemu ngumu zaidi itakuwa ni kukatisha katika bahari za Atlantic na Pacific safari inayoweza kuchukua siku tano mchana usiku.
TAZAMA VIDEO YAKE HAPA CHINI