Noma sana!! WALIMU ZAIDI YA 100 WAMFUNGIA OFISINI MKURUGENZI WA HALMASHAURI WAKIDAI PESA ZAO


Zaidi ya walimu 100 wanaofundisha katika shule za msingi na sekondari Wilaya ya Igunga, jana walimfungia ofisini Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Sisti Kessy kwa zaidi ya saa tatu wakimshinikiza kuwalipa mishahara yao ya mwezi Aprili na Mei mwaka huu wanayoidai.
Uamuzi huo ni sawa na ule waliyoufanya mwanzoni mwa mwezi huu baada ya kuwafungia Mkurugenzi Mtendaji, Rustica Turuka na Mkuu wa Wilaya hiyo, Elibariki Kingu ambaye aliwaahidi watalipwa pesa zao Ijumaa tarehe 13 muda ambao umepita.
Mwalimu John Ambele alisema, wameamua kumfungia ofisini Kaimu Mkurugenzi huyo ili ujumbe uweze kufika mamlaka husika, kwani wamechoka na ahadi za uongo zinazotumiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Rusctika Turuka.
Hata hivyo pamoja na walimu hao kuchukua uamuzi huo waliendelea kumhoji juu ya hatima ya mishahara yao, ukosefu wa mishahara yao ya mwezi AprilI na Mei, huku wakihoji hatua ya kusumbuliwa kutolipwa mishahara yao waliyokwisha itumikia kwa miezi hiyo.
Kufungiwa ofisini kwa ofisa huyo kuliwalazimu baadhi ya wakuu wa idara kupiga simu Polisi kuomba msaada na muda mfupi gari la Polisi liliwasili likiwa na polisi wa Kikosi Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa na mabomu ya machozi wakiwa na Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Igunga Aziz Mayunga.
via>>mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post