RAIS ALAZWA HOSPITALINI KWA UCHUNGUZI WA KIAFYA

Rais Zuma anatarajiwa kupumzika kwa muda kabla ya kurejea kazini
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amelazwa hospitalini kwa uchunguzi wa kiafya .

Taarifa hii ni kwa mujibu wa maafisa kutoka kwa ofisi yake. 

Taarifa hiyo ilisema kuwa Zuma atalazimika kumpumzika kwa muda ingawa ataendelea na majukumu yake ya kitaifa akiwa nyumbani.

Bwana Zuma ambaye alihusika na harakati dhidi ya utawala wa kibaguzi, ana umri wa miaka 72 na aliapishwa kwa muhula wa pili baada ya uchaguzi mkuu tarehe 24 mwezi Mei, ambapo chama chake ANC kilishinda uchaguzi huo.

“Hapo jana Ijumaa Rais Zuma alishauriwa kupumzika hasa baada ya msimu wa uchaguzi kukamilika wiki chache zilizopita.Madaktari hawajaeleza wasiwasi wowote kuhusu afya yake.’’

Baraza lake la mawaziri, lina kibarua kigumu kukabiliana na uchumi wa nchi hiyo unaoendelea kudorora kila kukicha pamoja na ukosefu wa ajira.
Wadadisi wanasema asilimia 25 ya wananchi hawana ajira.

via>>bbc

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post