Wimbo unaitwa "Ngoja Nijaribu" umeimbwa na msanii Paul Nicholaus maarufu kwa jina la "Peace Pozi" kutoka Shinyanga mjini akimshirikisha Mwakanjuki na Z H wote wakiwa ni wasanii kutoka Shinyanga.Huu ni wimbo wa pili wa msanii Peace Pozi wimbo wake wa kwanza unaitwa "Military Soldier" zote zimerekodiwa katika studio ya More Rhymes Adition Record ya mjini Shinyanga.
Ngoma hii kali inatambulishwa rasmi mchana huu na mtangazaji Steve Kanyefu maarufu MWANAPORII ama bwana Michapo kwenye kipindi cha Wasanii wetu kinachorushwa na Radio Faraja Fm Stereo ya Shinyanga
Peace Pozi ni miongoni mwa wasanii wachanga wanaofanya vizuri katika tasnia ya muziki hapa nchini Tanzania wasiliana naye kwa simu namba 0762 654 210.
Sasa Sikiliza ngoma hii kali ya Peace Pozi inaitwa "Ngoja Nijaribu" iko hapa chini
Social Plugin