Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TAZAMA PICHA-JENGO LA GHOROFA LINALOTISHIA MAISHA YA WATU MJINI SHINYANGA ,HOFU YATANDA WANANCHI KUANGUKIWA KAMA DAR ES SALAAM


Jengo la ghorofa linalojengwa mjini Shinyanga karibu na benki ya NMB Manonga linalodaiwa kutokidhi viwango hivyo kutishia maisha ya watu walio karibu na jengo hilo kwani kuna nyufa zimejitokeza na kusababisha wananchi kuhofia kukutwa na majanga kama yaliyokea jijini Dar es salaam baada ya ghorofa kuanguka na kusababisha maafa.



Ujenzi wa jengo hilo umeanza mwaka 2013.Kufuatia malalamiko ya wananchi,naibu meya wa manispaa ya Shinyanga leo ameamua kufika katika jengo hilo na kujionea nyufa zikiwa zimewekewa plasta kuziba zisionekane

Muda mchache baada ya kufika katika jengo la ghorofa linaloendelea kujengwa mkabala na benki ya NMB Manonga mjini Shinyanga wakati wa ziara ya siku moja na naibu meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila iliyolenga kukagua majengo ya serikali na watu binafsi akiwa ameambatana na mhandisi wa majengo katika manispaa ya Shinyanga  Steven Manyango(wa kwanza kulia).Katika ziara yake hiyo naibu meya David Nkulila ameagiza kusitishwa mara moja ujenzi wa ghorofa hilo linalojengwa na  na mkandarasi CMG Singher kutoka jijini Mwanza kutokana na kutokidhi viwango vinavyotakiwa kwani pamoja na kwamba ujenzi wake bado unaendelea lakini kuna nyufa na zimewekwa plasta 
Kufuatia kuwepo kwa mashaka na jengo hilo naibu meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila ameagiza ujenzi huo usitishwe kwa muda na kwamba jengo hilo litakaguliwa ili kuangalia kama linakidhi viwango au la.

Amesema atawasiliana na ofisi ya katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga kuja kukagua jengo hilo kutokana na kutokuwa na imani na mainjinia wa manispaa hiyo huku akiongeza kuwa watumishi hao wa serikali wamekuwa wakikaa kimya kwani miradi mingi inajengwa chini ya kiwango pengine wanapewa pesa ili wakae kimya.
Nkulila ameeleza  kutoridhishwa na utendaji kazi wa mainjinia wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga ambao wamekuwa kimya na kuruhusu ujenzi wa jengo hilo kuendelea 


Naibu meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila akiangalia nyufa iliyozibwa kwa simenti katika moja ya kuta za jengo hilo

Kulia ni mmiliki wa jengo hilo bwana Biku Bhati mkazi wa mjini Shinyanga ambaye amesema ujenzi huo umeanza mwaka 2013  na bado unaendelea na kwamba kama mmiliki hana wasiwasi kuhusu ujenzi wa ghorofa hilo kwa liko imara japokuwa tatizo liko kwenye plasta/lipu lakini kolamu (base) iko imara.

Katika ziara yake naibu meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila amekagua pia ujenzi wa nyumba ya watumishi katika Zahanati katika kijiji cha Bushola kata ya Mwamalili ambayo ujenzi wake bado unaendelea

Wanakagua ujenzi wa zahanati-Mbele ni naibu meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila,nyuma yake ni mhandisi wa majengo katika manispaa ya Shinyanga  Steven Manyango 

Ukaguzi wa jengo unaendelea-Jumla ya shilingi milioni 23 na laki 7 na nusu zimetumika katika ujenzi huo kati ya shilingi milioni 25 zilizotolewa na serikali katika awamu ya kwanza

Jengo la zahanati ya Bushola nalo limekutwa na nyufa kama unavyoona pichani.

Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com