TAZAMA PICHA KINACHOENDELEA KATIKA MANISPAA YA SHINYANGA


Katika pitapita zake kamera za Malunde1 Blog zimenasa ujenzi wa barabara mbalimbali katika manispaa ya Shinyanga japo barabara hizo hazijengwi kwa kiwango cha lami.Hapa ni katika barabara ya Oxfam mkabala kabisa na barabara ya Magadula inayotenganisha kata ya Ngokolo na Ndembezi.Barabara hii inatoka eneo la Oxfam na kuishia kwenye barabara ya Kalogo.Pichani ni tinga tinga likisambaza vifusi katika barabara hiyo

Ndiyo barabara ya Oxfam inayotoka barabara ya Magadula na kuishia kwenye barabara ya Kalogo mjini Shinyanga.Barabara hii ina mtaro mmoja pekee hivyo jitihada za maksudi zinahitajika kuweka mtaro mwingine wa kupitishia maji ya mvua kwani barabara hiyo hugeuka mto pindi mvua zinaponyesha

Ndiyo barabara yenyewe


Kushoto ni mtaro wa kupitishia maji ya mvua,upande wa kulia hakuna mtaro hali ambayo ni changamoto kwa uhai wa barabara hiyo

Hii ni barabara ya Fanta Video kama wenyeji wa eneo hilo wanavyoiita ambayo iko mkabala kabisa na shule ya msingi Bugoyi A na B katika kata ya Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga ambayo leo imemwagiwa maji 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post