Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TAZAMA PICHA TULICHOKIONA LEO MJINI SHINYANGA

Haya ni maji machafu yanayodaiwa kutiririka kutoka hospitali ya mkoa wa Shinyanga ambayo hupita kwenye mtaro nyuma ya shule ya Sekondari Buluba.Maji hayo machafu yamekuwa yakitiririka kwa zaidi ya miezi mitatu sasa ambapo wakazi wa maeneo yanakopita maji hayo wamedai kukerwa na harufu mbaya ya maji hayo huku wengine wakihofia kuripuka kwa magonjwa


Huu ni mfereji ama mtaro unaipitisha maji hayo yanayodaiwa kutoka hospitali ya mkoa wa Shinyanga na maji hayo huishia kwenye mto unaopita karibu na Shule ya sekondari Buluba ya mjini Shinyanga

Hapa ni kwenye daraja la barabara ya Magadula mjini Shinyanga ambapo kuna daraja ambalo chini yake ndiyo unapita mto ambao umekuwa suluhisho la maji machafu yanayodaiwa kutoka hospitali ya mkoa wa Shinyanga na kutishia maisha ya wapita njia na wakazi wa eneo hilo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com