|
Ni ndani ya ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga mjini Shinyanga-Aliyesimama ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akifungua warsha ya siku moja leo kuhusu mkakati wa kupunguza vifo vya mama na mtoto wa siku 600,ikiwa ni katika kutekeleza agizo la rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania alilolitoa Mei 15 mwaka huu.Pamoja na mambo mengine Rufunga alisema mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa inakabiliwa na changamoto ya vifo vya mama na mtoto lakini pia mkoa huo huo ni miongoni mwa mikoa 8 yenye maambuzi makubwa ya VVU lakini pia ni miongoni mwa mikoa 6 yenye changamoto kubwa ya ugonjwa wa malaria hapa nchini
|
|
Wa kwanza kulia ni katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Anselim Tarimo,katikati ni mwakilishi wa meya wa manispaa ya Shinyanga bi Mariam Nyangaka akifuatiwa na mwakilishi wa UNFPA bwana Rutasha Dadi wakiwa ndani ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga |
|
Wajumbe waliohudhuria warsha hiyo wameazimia mambo kadha wsa kadha ikiwemo kila halmashauri kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuchangia damu,wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii,kila mama mjamzito,anayenyonyesha pamoja na watoto kuwa wanapimwa VVU,pamoja na kila halmashauri kutunga sheria ndogo ili wanawake wajawazito wajifungulie katika vituo vya afya |
|
Wajumbe wa warsha hiyo pia walipendekeza kufunguliwa kwa vituo vyote vya afya vilivyofunguliwa na kuhakikisha dawa muhimu zinapatikana katika vituo vya afya ili kupunguza vifo vya mama na watoto. |
|
Wajumbe hao pia walieleza kukerwa na baadhi ya watumishi katika zahanati na vituo vya afya kutumia lugha chafu kwa akina mama wajawazito wanaofika eshemu hizo ambao wamekuwa wakitukanwa na baadhi ya watumishi hao |
|
Wajumbe wa warsha hiyo pia walipendekeza watumishi katika vituo vya afya na hospitali kulipwa vizuri kwani hivi sasa baadhi ya watumishi wameanza kujiingiza katika siasa |
|
Mwakilishi wa UNFPA bwana Rutasha Dadi akizungumza katika warsha hiyo ambapo hivi sasa mkoa wa Shinyanga umebadilika ukilinganisha na siku za nyuma hivyo kuwataka wadau mbalimbali kuungana kwa pamoja katika kupiga vita vifo vya akina mama na watoto |
|
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe akiwasilisha mada kuhusu mikakati ya mkoa wa Shinyanga katika kukabiliana na vifo vya akina mama na watotot |
|
Mmoja wa wajumbe akichangia mawili matatu katika warsha hiyo |
|
Warsha inaendelea |
|
Warsha inaendelea |
Picha ya pamoja kwa washiriki
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com