TAZAMA PICHA-WATOTO WENYE ULEMAVU KITUO CHA BUHANGIJA SHINYANGA WAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA
Sunday, June 15, 2014
Hapa ni katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga ambapo leo Jumapili Juni 15,2014 wameadhimisha siku ya mtoto wa Afrika ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 16 Juni,ambapo wao wameamua kufanya siku moja kabla kwa kukutana na waandishi wa habari pamoja na wadau wengine wa maendeleo wakiwemo maafisa kutoka shirika la kutetea haki za watoto la Erricks International
Wa pili kutoka kushoto ni bwana Peter Ajali mwalimu mkuu wa Shule ya Buhangija Jumuishi ambayo inalea watoto wenye ulemavu wa aina mbalimbali kama vile wasioona,wasiosikia na wenye ulemavu wa ngozi(albino).Mwalimu Ajali alisema miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo ni pamoja
na watoto hao kukosa daktari maalum kwa ajili ya kuhudumia watoto hao wenye
ulemavu.Ajali aliongeza hivi sasa kituo hicho kinalea
watoto 36 wasioona,48 wasiosikia na wenye ulemavu wa ngozi 180
Watoto wenye ulemavu wa ngozi,wasiosikia na wasioona wakiimba wimbo wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika kituo hicho cha Buhangija
Watoto wakifuatilia kilichokuwa kinajiri katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika
Aliyesimama ni mwenyekiti
wa baraza la watoto wenye ulemavu mkoa wa Shinyanga Bundala Habi ambaye aliitaka serikali kuwakamata watu wanaoagiza watu kukata viungo
vya watu wenye ulemavu tofauti na ilivyo sasa kwani wanaokamatwa ni wale
wakataji tu huku waliowatuma kukata wakiwa hawafuatiliwi.
Mwenyekiti wa baraza la watoto wenye ulemavu mkoa wa Shinyanga Bundala Habi pia aliitaka jamii kuwa na mtazamo hasi kuhusu watoto wenye
ulemavu kwani katika baadhi ya maeneo familia zimekuwa zikiingia kwenye
migogoro pindi anapozaliwa mtoto mwenye ulemavu,matokeo yake wanatekelekeza
watoto na hata kufikia hatua ya kutupa watoto hao.
Aliyesimama ni katibu wa baraza la watoto wenye ulemavu mkoa wa Shinyanga Mkama Shakeng'wa akizungumza katika maadhimisho hayo ya siku ya mtoto wa Afrika ambapo alieleza kukerwa na majina mabaya wanayopewa watu wenye ulemavu akitolea mfano wa Wasukuma ambao huwaita" Mbilung'wilu" na wengine kuwaita zeruzeru badala ya kuwaita ALBINO,ambapo alitumia fursa hiyo kuiomba serikali kuwachukulia hatua za kisheria
Waandishi wa habari wakiwa katika eneo la tukio
Mwandishi wa habari wa Star Tv Shaaban Alley akiuliza maswali wakati wa maadhimisho hayo
Afisa ushawishi na utetezi kutoka shirika la kutetea
haki za watoto la Erricks International bwana Josephat Torner alisema watoto
wenye ulemavu wanapaswa kupatiwa haki zao kama inavyotakiwa ikiwa ni pamoja na
kupatiwa matibabu bure.
Mwandishi wa habari wa Idhaa yaKiswahili yaDW Dotto
Bulendu akifuatilia kilichokuwa kinaendelea katika kituo cha kulelea watoto
wenye ulemavu cha Buhangija kilichopo katika manispaa ya Shinyanga kikiwa
kinakabiliwa na upungufu wa mabweni ambapo sasa watoto hao wanalazimika kulala
zaidi ya mmoja katika kitanda kimoja.
Mwandishi wa habari mkongwe hapa nchini Anikaz Ndaji
Kumbemba akipiga stori na watoto wenye ulemavu katika kituo cha Buhangija mjini
Shinyanga.
Mwandishi wa habari wa Idhaa yaKiswahili yaDW Dotto
Bulendu akiongea mawili matatu na watoto wenye ulemavu wa ngozi katika kituo
cha Buhangija mjini Shinyanga leo ambapo watoto hao na wale wenye ulemavu wa
macho(wasioona) na wasiosikia wameadhimisha siku ya mtoto wa Afrika mwaka 2014
kwa kukutana na waandishi wa habari.
Hili ni jengo linaloendelea kujengwa katika kituo cha Buhangija ambalo sasa watoto wenye ulemavu wanalazimika kulala kutokana na upungufu wa mabweni ukilinganisha na idadi ya watoto katika kituo hicho,na sasa yanahitajika mabweni 2 ya wavulana na moja la wasichana.
Hapa ni ndani ya jengo kama unavyoona chumba kikiwa
kinatumika pamoja na kwamba jengo halina mlango.Mkuu wa shule ya msingi Buhangija Peter alisema mbali na kituo cha Buhangija kukabiliwa na changamoto ya mabweni alisema hivi sasa watoto wenye ulemavu wa ngozi
katika kituo hicho wameongezeka kufuatia mauaji ya mtu mwenye ulemavu mkoani
Simiyu ambapo siku chache tu baada ya mauaji wamepokea watoto 7 wenye ulemavu
wa ngozi.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 Blog- Shinyanga
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin