TAZAMA PICHA-WAZIRI WA AFYA ATEMBELEA HOSPITALI YA MKOA WA SHINYANGA NA ILE YA WILAYA YA KISHAPU



Waziri wa afya na ustawi wa jamii nchini Dkt Seif Rashid akiwa amembeba mtoto aliyezaliwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga mara baada ya kutembelea wodi ya wazazi waliojifungua kwa njia ya upasuaji wakati wa ziara yake ya siku moja juzi Ijumaa mkoani Shinyanga  na pembeni yake ni mbunge wa jimbo la Kishapu Suleiman Nchambi.
 


Mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku akimpatia waziri wa afya na ustawi wa jamii Dkt Seif Rashidi taarifa ya afya kuhusiana na changamto walizonazo katika wilaya hiyo.
 


Kituo cha afya kilichopo kata ya Kishapu ndicho kinachotumiwa kama hospitali ya wilaya baada ya kukosa  hospitali ya wilaya ikiwa kinakabiliwa na changamoto za uhaba wa maji,msongamano wa wagonjwa na umbali mrefu wananchi kupata matibabu ikiwemo ukosefu wa dawa na vifaa tiba,ambapo kituo hicho cha afya kilijengwa mwaka 1940 na miundombinu yake imeonekana kuwa chakavu.
 


Mganga mkuu wa wilaya ya Kishapu Dkt Daniel Nsaningu akisoma taarifa na mikakati iliyopo ya kuondoa changamoto zilizopo katika wilaya hiyo za afya ambapo alieleza kuwa wilaya hiyo haina hospitali ikiwa mikakati iliyopo ujenzi unaendelea na tayari baadhi ya majengo yamekwisha kamilika.
 


Mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku akitoa taarifa ya wilaya yake kuhusu  changamoto ya upande wa afya kwa waziri wa afya Seif Rashid alipokuwa katika ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo na kabla ya hapo alisaini kitabu cha wageni ndani ya ofisi hiyo.
 



Waziri wa afya akijibu changamoto zinazowakabili kwa upande wa afya wilaya ya Kishapu ambapo walieleza kukosekana na hospitali ya wilaya imesababisha vifo vinne vya mama wajazito na watoto wapatao 105 kutokana na umbali mrefu wa kupata huduma ya afya wilayani humo.
 



Hili ni jengo la wagonjwa wa nje (OPD) ambalo limejengwa kwa gharama ya shilingi millioni 291 mpaka hapo lilipofikia.
 



Hii ni moja ya wodi ya wagonjwa katika hospitali ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga mara baada ya waziri wa afya kutembelea ujenzi huo ambao bado haujakamilika kwa baadhi ya majengo.
via>>sungwakareny
blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post