MTOTO mmoja wa kike amefariki dunia mkoani Kilimanjaro baada ya kubakwa na Baba yake mzazi.
Akidhibitisha kutokea kwa tukio hilo la kinyama, Kaimu Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Koka Moita, alisema tukio la ubakaji lilitokea wilaya ya Karatu, mkoani Arusha, kabla ya kufariki kwake mjini Moshi.
Alisema wakiwa huko Mang’ola baba huyo aitwae Elisha Wazaeli, (38), alimbaka mtoto huyo kabla ya kurudi nae nyumbani kwao Arusha na kwamba alipofika Arusha alikorofishana na mke wake ambae ni mama wa mtoto huyo.
Aliendelea kusema kuwa pamoja na kupewa dawa lakini homa hiyo iliendelea kumuandama mtoto huyo na baada ya mamake kumhoji zaidi alimwambia mamake ya kuwa babake alimbaka.
Kaimu Kamanda Moita aliendelea kusema kuwa polisi walimchukua mtoto huyo na kumpeleka hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi pamoja na tiba katika hospitali ya Mkoa ya Mawenzi hadi alipofariki dunia Juni 4, mwaka huu.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda huyo, mtuhumiwa wa tukio hilo ametoroka na kwamba tayari jeshi la polisi mkoani humo limeanza msako wa kumtafuta ili hatua za kisheria zichukue mkondo wake.
Aidha Kaimu Kamanda Moita alitoa wito kwa akina mama kuhakikisha wanakuwa karibu na watoto wao badala ya kuwaachia wafanyakazi wa nyumbani jukumu hilo muhimu katika malezi ya watoto.
Social Plugin